Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
MGOMBEA wa nafasi ya ubalozi wa nyumba 10 shina namba 6 Tandale kwa Mkunduge kupitia tiketi ya CCM amepita bila kupingwa katika zoezi la uchaguzi uliofanyika kwenye kiwanja cha Kameroon Mkoani Dar es Salaam.
Hatua hiyo imekuja mara baada ya MGOMBEA huyo Bi Kijakazi Waziri kujikuta akiwa hana mpinzani kwa kujizolea jumla ya kura 48 za ndio kwa wakazi hao,ambapo nafasi ya kiti hicho huwapa fursa viongozi kuweza kuongoza kwa kipindi cha miaka mitano.
Akizungumza Mkoani humo Mgombea wa kiti hicho Bi Kijakazi Waziri amesema kutokana na kuaminika kwake amewaomba wakazi hao kushirikiana kwa pamoja katika masuala mbalimbali yaliyomo ndani ya jamii na Taifa kwa ujumla.
“Ushindi huu sio wa kwangu peke yangu ila ni wa wote, naomba ushirikiano wenu katika kubaini changamoto zilizomo katika maeneo yetu cha msingi ni utoaji wa taarifa kwa wale wenye nia ya kukwamisha jitihada za Rais wetu,” amesema Bi Kijakazi
Kwa upande wake msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) kata hiyo Bi Zena Abdallah Kigodi ameeleza kwa miongoni mwa mashina 10 yaliyofanya uchaguzi katika eneo hilo . Hata hivyo Mgombea wa shina hilo amepita bila kupingwa kwa kukosa upinzani.
Kiongozi huyo amewasihi wakazi hao kuwa na tabia ya kujitokeza katika mikutano mbalimbali pia amewahimiza kujitokeza katika nafasi za chaguzi za viongozi kwa lengo la kuisaidia Serikali kwani kupiga kura ni haki ya kila mmoja wetu.
Nae msaidizi wa balozi huyo aliyejulikana kwa majina Mwajuma Mussa amewataka wananchi wa Mkunduge kutii Sheria za viongozi wao kuwa pamoja na viongozi waliopewa dhamana ya kuwatumikia kwenye mitaa waishiyo.
More Stories
Wassira:Waliopora ardhi za vijiji warudishe kwa wananchi
Rais Samia apongezwa kwa miongozo madhubuti ya ukusanyaji wa kodi
Mwenda:Siku ya shukrani kwa mlipakodi ni maalum kwaajili ya kuwatambua,kuwashukuru