January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea uspika ADC aahidi makubwa, arudisha fomu kwa kishindo

Na David John, TimesMajira Online

MGOMBEA wa kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano waTanzania kwa tiketi ya Chama cha Alliance Democratic Change ADC Maimuna Said Kassim amerudisha fomu kwenye ofisi za chama hicho Buguruni nakudai kwamba ameamua kugombea kwasababu anasifa za kuwa Spika.

Amesema kuwa ana elimu ya kutosha na ameshika nafasi mbalimbali za uongozi ikiwamo kuwa mbunge wa wanafunzi chuo kikuu cha Dodoma hivyo anauzoefu wa kutosha na hana mashaka na uwezo wake.

Maimuna ameyasema haya jijini Dar es Salaam katika ofisi chama hicho zilizopo buguruni jijini humo ambapo Amesema amerudisha fomu hiyo ili chama chake kiweze kutoa ridhaa ya yeye kugombea kiti hicho na anaamini mambo yatakuwa mazuri.

” Nilichukua fomu na leo nimerudisha kwani mwisho wa kuchukua fomu na kurudisha ni January 20 mwezi huu hivyo nami nilichukua na leo nimerudisha kikubwa nikwamba nimejipanga vema na niko tayari kwa kinyang’anyiro hiki cha uspika.”amesema Maimuna

Ameongeza kuwa endapo chama chake kikiridhia jina lake kupeperusha bendera na pia katika kinyang’anyiro akifanikiwa kupita na kuwa Spika atahakikisha anaondoa migongano ambayo wakati mwingine inajitokeza.

Kwauapnde wake kaimu naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Donni Mnyamani akizungumzia urejeshaji wa fomu hiyo Amesema mgombea Maimuna alichukua fomu ya kugombea uspika na sasa amerejesha na wao Kama Chama wamepokea na taratibu zingine zitafuata.

Amesema kuwa Maimuna ndio mwanachama pekee ambaye amechukua fomu hadi kufikia leo lakini wanapokea mwanachama yeyote ambaye anataka kuchukua fomu ajitokeze kwani mchakato huo unafungwa januari 20 mwaka juu.

Ameongeza kuwa Kama hadi kufikia siku hiyo hakuna atakayejitokeza niwazi kwamba Mauimuna atakuwa ndio mwanachama pekee ambaye amechukua fomu ndani ya chama hicho.

“Tumepokea fomu hii saa 10.40 nasisi baada ya kupokea utaratibu mungine utafuata ndani ya chama ila Kama Chama tunampongeza na kumshukuru kwa hatua hii.” Amesema Donni

Kiti cha uspika kipo wazi kufuatia aliyekuwa Spika wa Bunge la Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Job Ndugai kujiudhuru kutokana na changamoto mbalimbali.

kaimu katibu mkuu wa chama cha Alliance Democratic Change akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusu kurejesha fomu ya usipika mwanachama wa chama hicho Maimuna Kassim.
Maimuna Kassim akirejesha fomu ya usipika kwenye Makao makuu ya chama cha ADC Buguruni jijini ambapo imepokelewa na Kaimu katibu mkuu wa ADC Donni Mnyamani