March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea Urais Chama Cha Makini achukua Fomu Tume,akishinda ahaidi ekari tano kwa kila kijana

Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma

COASTER Kibonde na Mgombea Mwenza Azza Haji Suleiman kutoka Chama Cha Makini (MAKINI)amekuwa mgombea wa nne kuchukua fomu ya kugombea Urais katika Ofisi za Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC)toka kutangazwa kwa ratiba ya uchukuaji fomu. 

Mara baada ya kuchukua Fomu jijini hapa leo Agosti 10 ,2025 ,Njedengwa zilipo Ofisi za Tume hiyo Kibonde alizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema Chama hicho kinaviapaumbele vitatu ambavyo ni Elimu ,Kilimo na Afya.

Amesema kuwa Ndani ya Chama Cha Makini wanaenda kufanya kilimo cha kumkomboa mtanzania ambapo ameahidi kuwa  kwa Watanzania ambao ni vijana waliotimiza umri wa miaka 21 kwamba kila kijana kwa yale maeneo ambayo yatapatikana mashamba,tofauti ya mjini  kila kijana atampatiwa hekari tano kwajili ya kufanya kilimo na kilimo ambacho kitakiendeshwa chini ya serikali ya chama hicho ni kilimo chakutumia mashine.

“Kuhusu masuala mazima ya kilimo,sisi kilimo ndiyo mahali petu na ndiyo maana ukiangalia makini ni kifupi na kirefi chake ni Maarifa,Kilimo na Nishati.

“Tumefanya ziara wiki mbili zilizopita,Katibu Mkuu na baadhi ya viongozi walikwenda India,wamekwenda kujifunza,masuala mazima yanayohusiana na kilimo,”amesema.

Amesema kuwa Suala la elimu watafanya jitihada za makusudi kuhakikisha kijana wa Tanzania anapata Elimu yoyote inayopatikana Duniani kokote.

“Tunaanza na Elimu,imani yetu sisi kama Chama Cha Makini tunasema kwamba ukimnyima Mtanzania yeyote elimu ni sawa na kama umemfunga jela kifungo cha maisha na ndiyo maana tunasema,sisi kwa suala la elimu tutalivalia njuga na tutaliweka kipaumbele tukiamini ya kwamba bila elimu hakuna jambo lolote linaloweza kufanyika katika nchini ya Tanzania kwa maslahi ya Tanzania na kuindeleza nchi yetu,

“Serikali ya Chama cha Makini itawapeleka vijana wake nje ya nchi lengo ni kwenda kupata Elimu,wakishapata Elimu watarudi nyumbani wakiwa na ujuzi kamili,”amesema.

Kwenye Suala la Afya,amesema unasema kwamba imani yao inasema kiwa kumnyima Afya Mtanzania ni sawasawa na kumuhukumu  kifo.

“Kwa hivyo basi serikali ya Chama cha Makini,tunasema ni Serikali ya matumaini mapya kwa Watanzania tutakwenda kujenga vituo vya afya kila Kata na siyo tu kujenga vituo vya afya kila kata tutahakikisha kwamba vifaa tiba kila hospitali ambayo itakwenda kujengwa tutaweka vifaa tiba,”amesema.

Na vilevile kwa wakati huo huo kwakuwa tunaamini katika suala zima la Elimu tutahakikisha Madaktari wa kutosha,wauguzi wakutosha kwahiyo tuaamini kwamba maeneo yote tutatawanya wahudumu ambao watakwenda kutoa tiba kwa watanzania.

“Na tiba yetu tumesema kwamba,Serikali ya Chama cha Makini tutaanzisha bima ya Afya ambayo tumeshaipatia  jina tunaita ‘MAKINI CARE’ambayo ile bima itakuwa ni bima kwa kila Mtanzania maana yake watanzania wote wataelea katika hiyo bima ya Afya ambayo itakuwa ni bima ya serikali ya Chama cha Makini.

Pamoja na hayo amesema kuwa yeye Kama Mgombea wa Chama Cha Makini amependezwa  na maandalizi ya Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi.

“Wanamaandalizi mazuri,wametupokea vizuri na michakato yao ni mizuri hivyo basi   tarehe 29,Oktoba watanzania wajitokeze kwa wingi wakapige kura na hatimae mimi nina imani ninaenda kuwa mshindi Nintendo kuunda serikali ya chama cha Makini