December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea urais ADC aahidi kurejesha kiwanda cha kuzalisha gesi Mtwara

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira Online, Mtwara

“MKINIPA kura za kutosha Oktoba 28 nawaahidi kurudisha kiwanda cha kuzalisha gasi hapa mtwara ili watoto wetu, vijana wetu nao wanufaike na rasimali hii Mungu aliyetuzawadia ” 

Hiyo ni kauli ya mgombea wa urais kwa chama cha ADC Queen Sendiga alipokuwa akizungumza wananchi wakati wa kuhitimisha kampeni zake katika Wilaya Tandahimba katika kijiji cha Nanyagaa hivi ambapo sasa ataendelea na kampeni zake Wilaya ya Rufiji, Kibiti na Mkuranga.

“Jukumu lingine kubwa kwa Serikali makini inayojali maisha ya watu ni kupanga namna njema ya matumizi ya rasilimali zilizopo kwenye maeneo/mikoa husika kwa manufaa ya wakazi wake

ADC ikipata nafasi ya kuongoza nchi inaahidi kurejesha ujenzi wa kiwanda cha gesi hapa Mtwara kama Serikali ilivyoahidi wananchi wa Mtwara awali na baadae ikafanya tofauti bila kuwashirikisha

Baadhi ya wananchi waliofika kusikiliza sera za chama hicho wakati mgombea urais wa ADC Queen Sendiga akizungumza.

Ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kutasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana,uhakika wa umeme na upatikanaji wa gesi ya gharama nafuu kwa matumizi ya majumbani 

Pia mgombea alipata nafasi ya kuwanadi madiwani wa Kata za Mdimba, Mikunda na Kwanyama