Na Bakari Lulela, TimesMajira Online
MGOMBEA uenyekiti wa chama cha (ADC) Doyo Hassan Doyo amekata rufaa dhidi ya mpinzani wake katika uchaguzi wa chama hicho ulifanyika Juni 30 mwaka huu katika ukumbi wa Lamada jijini Dar es salaam.
Rufaa hiyo imekuja baada ya uendeshwaji wa uchaguzi kutawaliwa na vitimbi vya kuwakingia kifua baadhi ya wagombea Ili wawezekushinda.
Uchaguzi ambapo ulitawaliwa na sintofahamu pamoja na ukiukwaji wa Sheria na katiba za chama katika mkutano mkuu wa chama hicho.
Akizungumza jijini Doyo Hassan Doyo amesema kulingana katiba ya chama chao, uchaguzi ule ulikuwa batili kwa kuwa haukufuata kanuni, miongozo na sheria za chama.
“Uchaguzi ule ulikiuka utaratibu mzima wa kanuni na Sheria kwa msimamizi wa uchaguzi kwenda kinyume na usimamizi vilevile wapiga kura hawakupewa nafasi stahiki ya kupiga kura kwa Siri,” amesema Doyo
Doyo amesema kuwa idadi ya majina ya wajumbe yaliyokwenda kwa msajili ni machache kulingana na idadi ya wajumbe katika kinyang’anyiro cha uchaguzi huo
Aliainisha kwa kutaja idadi stahiki ya wajumbe ilikuwa ni 192 lakini idadi ya kura zilipigwa ni 242 ambapo imeonekana kura 50 ni batili.
More Stories
Serikali kupeleka mawasiliano maeneo ya mipakaniÂ
Sekondari ya Butata mbioni kufunguliwa Musoma Vijijini
TIC yapongeza mradi wa Kampuni ya Big Best