Na Mwandishi wetu,Timesmajira
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Segerea kupitia chama cha ukombozi wa umma (CHAUMMA) Agness Leizer amewaahidi wakazi wa Jimbo hilo mara watakapo mchagua kushika kiti hicho atawaondolea changamoto za ukosefu wa maji pamoja na kuwapatia mkopo .
Akizungumza jana jijini Dar es salaam, katika mkutano wa kufunga kampeni za Ubunge zilizofanyika jimboni humo, amesema kuwa wakazi wa Jimbo hilo mtakapo mchagua yeye ataondoa kero mbalimbali zinazowakabili ikiwemo ubovu wa miundombinu, kuondoa tozo za taka taka zinazotozwa kiholela.
“Nipeni kura zenu ndugu wananchi Ili niwaondoleeni kero zinazowakabili, Chaumma ni chama Bora chenye muongozo sahihi katika kuwasaidia watanzania kupata haki zao za msingi ikiwemo maji safi na salama, huduma muhimu za kijamii na kuwajengea miundombinu rafiki ya barabara na masoko,” amesema Agness
Aidha Mgombea huyo ameyabeza Yale yote yaliyofanywa na Mgombea wa CCM kwa kutowafanyia wakazi wa Jimbo hilo katika kipindi cha miaka mitano kilichopita na kuahidi watakampatia ridhaa changamoto hizo kwake atazigeuza kuwa fursa kwa wakazi hao.

Agness amewapa matumaini mapya wakazi hao kwa kuwarahisishia huduma bora za afya kwa wamama wajawazito na wazee umri uliokwenda kupata huduma hizo bila gharama zozote zile.
Katika kampeni hiyo mamia ya wakazi wa Jimbo hilo walimiminika kwa wingi kusikiliza sera mbalimbali za Mgombea huyo sambamba na wagombea wengine ambao Agness waliwataka kujitambulisha mbele ya wapiga kura wao wakiwemo madiwani wa buguruni, Tabata na kuelezea namna sera zao zitakavyowaletea maendeleo wakazi hao.

More Stories
Clara:Miaka 50 ya Sabasaba fursa mpya za Biashara na Uwekezaji
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI