November 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meneja Kampeni wa CCM Jimbo la Ilemela Kazungu Idebe akimnadi Mgombea Ubunge kupita CCM Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula( kushoto) na mgombe udiwani Kata ya Kawekamo Omary Juma kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika uwanja wa stendi ya Pasiansi Kata ya Kawekamo.

Mgombea ubunge Ilemela awashauri wananchi kujinga na NHIF

Na Judith Ferdinand-TimesMajira Online,Mwanza

IMEELEZWA kuwa katika kipindi cha miaka mitano Serikali kupitia CCM imefanikiwa kuboresha sekta ya afya,hivyo wananchi wa Jimbo la Ilemela wamehimizwa kujiunga na bima za afya ili kupata huduma ya matibabu kwa urahisi na uhakika.

Mgombea ubunge kupita CCM Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika uwanja wa stendi ya Pasiansi Kata ya Kawekamo.Picha zote na Judith Ferdinand

Rais John Magufuli aliboresha huduma ya bima ya NHIF kwa kuanzisha kifurushi cha mtu mmoja mmoja bila kujali ajira yake pia CHF ilioboreshwa inayotoa fursa ya familia ya watu 6 kupata matibabu kwa kuchangia kiasi cha sh.30,000.

Hayo yamesemwa na Mgombea ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi(CCM), Jimbo la Ilemela,Dkt.Angeline Mabula wakati wa mkutano wake wa kampeni katika uwanja wa stendi ya Pasiansi Kata ya Kawekamo.

Wananachi wakimsilikiza mgombea ubunge kupita CCM Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula.

Amesema Serikali imeboresha huduma ya afya na matibabu yanapatika hivyo ni vyema sasa wakati tunapozungumzia uwekezaji pia wanazungumzia na uwekezaji katika afya,hivyo wananchi wakate bima ili wakati wowote wapate huduma.

“Hakuna mwenye mawasiliano na Mungu ya kujua lini ataugua na hatakua katika hali gani kiuchumi, kwa kulitambua hilo Serikali ya Dkt.Magufuli ilikuja na hoja ya msingi na nzito ya watu kupata huduma ya afya kulingana na kipato chao kupitia bima ya afya ya NHIF na CHF ilioboreshwa ambayo inatoa fursa ya familia ya watu 6 kutibiwa kuanzia ngazi ya zahanati hadi hospitali ya Mkoa kwa gharama ya 30000 kwa mwaka mzima,” amesema Dkt.Angeline.

Amesema kwa kuboresha sekta hiyo vifo vya mama na mtoto vimepungwa sana jimboni Ilemela na taifa kwa ujumla kwa sababu ya kuboresha huduma katika maeneo hayo pamoja na ongezeko la dawa ambazo zinapatikana kwa asilimia 98.

Hata hivyo aliwaahidi wananchi wa Kata ya Kawekamo kuwa endapo watamchagua Rais,Mbunge na diwani anayetokana na CCM na wakashinda katika uchaguzi mkuu kwa utaratibu ule ule wa tatu watajenga zahanati ya kata hiyo.

Meneja Kampeni wa CCM Jimbo la Ilemela Kazungu Idebe akimnadi Mgombea Ubunge kupita CCM Jimbo la Ilemela Dkt.Angeline Mabula( kushoto) na mgombe udiwani Kata ya Kawekamo Omary Juma kwenye mkutano wake wa kampeni uliofanyika uwanja wa stendi ya Pasiansi Kata ya Kawekamo.

Sanjari na hayo kupitia mkutano huo aliyekuwa Mjumbe wa Kamati Tendaji Wilaya ya Ilemela na Katibu Mwenezi Wilaya ya Ilemela wa CHADEMA Johanes Emmanuel,alijiunga na chama cha CCM kwa madai kuwa haoni sababu ya kubaki alipo kuwa wakati mambo yanayofanywa na CCM yanaonekana na kufurahishwa na utendaji kazi wa awamua ya tano.

“Tulikuwa tunadai vituo vya afya tumeshuhudia Serikali ya Awamu ya Tano ikijenga,miundombinu ikiboreshwa,usafiri wa majini ikiwemo kivuko cha MV.Ilemela, shule zimejengwa na kuboreshwa mfano kisiwa cha Bezi kulikua hakuna shule ila kupitia Dkt.Angeline sasa watoto wanasoma,nimeona aibu ndio maana nimerudi CCM,” amesema Emmanuel.