March 7, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgombea Ubunge aahidi mabadiliko Jimbo la Temeke

Na Bakari Lulela ,Timesmajira

Mtia nia wa Ubunge Jimbo la Temeke kupitia chama cha Mapindizi (CCM)Jasdeep Sindgh ameahidi kuleta Mabadiliko makubwa mara tu atakapopata ridhaa ya kuchaguliwa nafasi hiyo kwa kuwatumikia watanzania.

“Nimejenga vyumba nane katika wodi ya wazazi kwa ajiri ya wakina mama kwenda kujifungulia kwa pesa binafsi, nimejenga jiko  katika shule za misingi ambalo linahudumia watoto 1500  bila michango ya wazazi wao , nimejenga maktaba kwa shule ya sekondari kwa ajiri ya wanafunzi wetu kwa ajiri ya kujisomea”Amesema JASDEEP 

Aidha mtia nia huyo  SINGH eliendelea kwa kusema ametoa kadi za bima ya afya kubwa kutoka ufadhili wa ubalozi wa Marekani takribani kaya 77sawa na watu 560 .

Sanjari na hilo alipongeza ilani ya chama cha mapinduzi ( CCM)  kwa kuleta dira ya maendeleo ya mwaka 2050 hivyo itapelekea kuleta viongozi waadilifu, wachapa kazi wawazi na kuleta uongozi ambao unaleta maendeleo katika jamii zetu.