Na Zena Mohamed,Timesmajiraonline,Dodoma
GEORGES Bussungu anakuwa Mgombea wa saba kuchukua Fomu katika Ofisi za Tume huru ya Taifa ya Uchaguzi(INEC) kutoka African Democratic Alliance Party(ADA-TADEA) akiwa na mgombea mwenza Ali Makame Issa .
Mgombea huyo akiwa na Mgombea Mwenza walichukua fomu jijini hapa leo,Agosti 11,2025 Njedengwa zilipo Ofisi za Tume
hiyo ambapo walikabidhiwa mkoba wenye fomu za kuomba kuteuliwa kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi,Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele.



Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kuchukua fomu hizo Bussungu amesema kuwa Chama chao ni Chama ambacho kinamtazamo tofauti kuwa Mtazamo wao mkubwa ni usawa kwa jamii.
Ametaja nia kubwa ya kugombea Urais ni kuleta mabadiliko makubwa katika jamii ya wananchi wa Tanzania.
“Kitu cha muhimu ulimwengu umebadilika sasa ni ulimwengu wa akili mnemba au AI kwahiyo Chama cha ADA-TADEA mwelekeo wake ni kuleta mapinduzi makubwa ya Njano.
Kwahiyo mapinduzi ya njano yatashughulika na mapinduzi makubwa ya fikra,kubadilisha mapinduzi ya fikra,mapinduzi ya teknolojia na mapinguzi ya uchumi,”amesema.
Hata hivyo Bussungu aliwaambia waandishi wa habari kuwa ufafanuzi zaidi watapata baadae wakishamaliza kuteuliwa kama wao Wagombea Urais kupitia ADA-TADEA katika uchaguzi wa Taifa.Ambapo uteuzi rasmi utafanyika Agosti 27,2025.
Nitoe pole kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Chama cha Mapinduzi kwa msiba mzito uliotokea kwa Mhe.Job Yustino Ndugai,kwakweli chama cha ADA-TADEA kimesikitishwa sana na msiba wa Spika Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kinawapa pole sana familia ya Ndugai.






More Stories
Wanawake jumuia ya kikristo Tanzania CCT wafundana kuelekea siku ya Wanawake Duniani
Dkt.Tulia,Mwalunenge waungana kutatua changamoto ya barabara
TUCASA yaomba kuanzishwa sheria malipo sekta ya ujenzi