Na Heri Shaaban (CCM ILALA)
DIWANI MSTAAFU wa chama cha Mapinduzi CCM kutoka kata ya Kinyerezi Wilaya ya Ilala Leah Mgitu,amewataka wananchi wa Kinyerezi kumchagua Mgombea Udiwani wa kata hiyo John Ryoba Mrema (Wahenga)ili aweze kuleta maendeleo kwa wananchi wa Kinyerezi.
Leah Mgitu,alisema hayo kata ya Kinyerezi Dar es Salaam wakati wa kuwashukuru wananchi wa Kinyerezi katika vipindi viwili vya uongozi wake alivyowatumikia na sasa kijiiti cha uongozi anamkabidhi John Ryoba Mrema aliyeteuliwa na chama cha Mapinduzi kugombea Udiwani Kinyerezi.

“Nawashukuru wananchi wa Kinyerezi katika kipindi nilichokuwa Diwani wa Kinyerezi maendeleo makubwa yamefanywa na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kata ya Kinyerezi sekta ya afya,sekta ya Elimu na Miundombinu ya barabara yote hiyo ni kazi ya Dkt Samia katika utekelezaji wa Ilani ya chama cha Mapinduzi sasa naomba kura za Udiwani za Chama cha Mapinduzi kwa Diwani wetu John Ryoba Mrema ,Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ili waweze kuleta maendeleo hapa Kinyerezi “alisema Leah Mgitu.
Leah Mgitu ,amesema John Ryoba Mrema atakuja kufanya makubwa Kinyerezi kama alivyofanya yeye wamchague ili aweze kuibadirisha Kinyerezi zaidi kwa kisogeza huduma za kijamii kwa wananchi na kutatua kero mbali mbali.

Akielezea baadhi ya kero alizotatua akiwa Diwani wa kata ya Kinyerezi vivuko vya barabara kwa ushirikiano wa Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan ambapo wamejenga vivuko vyote kwa Majoka na barabara kiwango cha lami.
Akizungumzia sekta ya Elimu Serikali ya Dkt.Samia imejenga shule ya Msingi Kifuru ya kisasa ya viwango na wamependekeza iwe English Medium ili kupunguza umbali wa watoto kuwapeleka Daimond na Olimpio na madarasa wamejenga shule ya Zimbili na Kibaga na Kinyerezi Jica.
Akizungumzia upande wa Shule ya Sekondari alisema shule ya Hari wamevunja kwa sasa Serikali inajenga ya kisasa pamoja na Kisungu pia wanafunzi wa Kidato cha tano na kidato cha sita kwa sasa wanafunzi wanasoma Kinyerezi na mikakati ya Serikali wanatarajia kujenga kidato cha tano na sita golofa hivyo chagua ccm kwa maendeleo Kinyerezi.

Akizungumzia sekta ya afya alisema awali kulikuwa na Zahanati ndogo Kinyerezi ikitoa huduma za afya kwa sasa Serikali ya chama cha Mapinduzi CCM imejenga kituo cha afya cha kisasa kinatoa huduma zote za mama na Mtoto wananchi kwa sasa hawakimbilii Amana kujifungua badala yake wananchi wa Kinyerezi na Jimbo la Segerea wanajifungulia hapo.
Mgombea udiwani Kata ya Kinyerezi CCM JOHN RYOBA MREMA alisema atakapopata ridhaa kuchaguliwa na wananchi kipaumbele chake cha kwanza kutatua kero ya wananchi kujenga mtandao wa Barabara za ndani zikiwemo barabara ya sheli Puma ,kwa Ulimbanga,Kifuru Mtaa Kichangani alisema kabla ajapewa ridhaa kuwa Diwani baadhi ya barabara alikuwa anatengeza kwa pesa yake ikiwemo kumwaga zege.
Aidha John Ryoba Mrema alisema yeye atakuja kuwa Diwani wa kuleta maendeleo kero nyingine kata ya Kinyerezi kuwatua ndoo kichwani kina mama kwa kuwaondolea kero ya maji ya DAWASA
“Kipaumbele changu cha tatu kuja kutoa fursa kwa vijana wanawake na watu wenye ulemavu kwa kusimamia mikopo ya asilimia kumi ambayo inatolewa ngazi ya Halmashauri kwa ajili ya kukuza uchumi kwa wananchi wa Kinyerezi naomba wana Kinyerezi mnipe kura ya ndio pamoja na Mbunge wangu Bonah Ladslaus Kamoli na Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan tuweze kuleta maendeleo “alisema John Ryoba.
Akizungumzia kero ya Takataka kata ya Kinyerezi alisema atakapopata ridhaa kuingia madarakani kero ya Mkandarasi wa Takataka yote itakwisha Kinyerezi itakuwa safi na wananchi hawawezi kusumbuliwa kwa kukamatwa kamatwa kila wakati .
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ilala Said Sidde ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo aliwataka wananchi wa Kinyerezi kumchagua chama cha Mapinduzi CCM kwa ajili ya kuleta maendeleo kata ya Kinyerezi
“Chagua Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan amemaliza kero ya umeme katika nchi yetu kwa sasa umeme unapatikana wakati wote na mradi wa Mabasi ya Mwendo Kasi unakuja kutoka Kigogo mpaka Jimbo la Segerea ni kazi itafanywa na Serikali ya chama cha Mapinduzi katka utekelezaji wa Ilani wananchi kwa sasa wanasafiri na reli ya kisasa SGR Dar es Salaam mpaka Morogoro hadi Dodoma kwa siku hiyo unaenda na kurudi yote hiyo ni kazi ya Chama cha Mapinduzi ” amesema Sidde.

More Stories
Usajili wa Laini za Simu: Jilinde Dhidi ya Kutumiwa Vibaya kwa Utambulisho Wako
TTCL yaadhimisha siku ya Wanawake kwa kutoa msaada JKCI
Wananchi Dodoma washauri TBA kujenga nyumba za kupangisha watu binafsi