December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mgeja ataka elimu ya kilimo itolewe kwa vijana,kubadili mawazo kuwa kulima ni kama adhabu

Na Patrick Mabula, TimesMajira Online Kahama

Serikali imeombwa kutoa elimu ya kilimo kwa vijana ili waweze kuondokana na dhana potofu ya kuona kuwa kulima ni kama adhabu.

Ombi hilo limetolewa na Mwenyekiti wa Mzalendo Foudition na mkulima wa kata ya Kilago , wilaya ya Kahama , Khamis Mgeja,wakati akiongea na wakulima na maofisa ugani katika kijiji cha Lowa Kata ya Kilago,Manispaa ya Kahama.

Ambapo amesema kuwa kilimo kina fursa nyingi za kuweza kujiajiri huko vijijini badala ya kuwaacha wakakimbilia mijini inapaswa vijana wapewe elimu na wawezeshwe ili wajiajiri katika sekta hiyo ambayo itawasaidia kujikwamua kimapato na kuchangia pato la taifa.

Mkuu wa Idara ya kilimo wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama, Jeremiah Inegeja amesema kuwa sekta ya kilimo ina ajira nyingi mbalimbali zikiwemo za ufugaji na kuomba uwepo ushirikishwaji katika suala la kutoa elimu ili watu wasikichukie kilimo kutokana na mapokeo mabaya yaliyopitwa na wakati.

Mjumbe wa kamati ya mradi wa PETS , unaofadhiliwa na The Foundition for Civil Society wa Kata ya Igunda na kutekelezwa na Chama cha Wasioona Mkoa wa Shinyanga Charles Kafuku ameiomba serikali kuongeza kuajiri maofisa ugani weweze kuwasaidia watu katika suala la kuwapatia elimu ya kilimo chenye tija huko vijijini .

Kwa upande wake muwezeshaji katika mradi PETS katika mfumo wa ufatiliaji wa matumizi ya raslimali za umma katika sekta ya kilimo , Dickson Maganga amesema bado kuna changamoto nyingi katika suala la kilimo ikiwemo uelewa mdogo wa wakulima katika matumizi ya mbolea na upatikanaji wa pembejeo kwa wakati.

Mkulima wa kata ya Kinamapula , Emmanuel Andrew ameiomba serikali iwekeze elimu na teknolojia ya kilimo katika vichwa vya vijana ili iweze kuwasaidia kujiajiri na kwa upande wa pembejeo za kilimo ziweze kupatikana vijijini kwa wakati na Tanzania bila njaa inawezekana.

Mwenyekiti wa Chama cha wasioona mkoa wa Shinyanga , Marco Kanjiwa akiongea na Wakulima , na viongozi wa kata na baadhi ya maafisa ogani na wajumbe wa PETS wa Mfumo wa ufatiliaji wa matumizi ya raslimali za umma za kilimo katika kikao kilichofanyika kijiji cha Lowa kata ya Nyandekwa , Halmashauri ya Manispaa ya Kahama .
Mwenyekiti wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Mzalendo Foundition , Khamis Mgeja aliyekaa wa wa pili toka kushoto akiwa na wakulima , maafisa ugani na baadhi ya viongozi toka Kata za Nyandekwa ,Igunda , Kinamapula , na Bukomela za wilaya ya Kahama wanakotekeleza mradi wa PETS baada ya kikao kilichofanyika kata ya Nyandekwa.