January 10, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mfungwa atuhumiwa kumbaka mtoto wa miaka 14

Na George Mwigulu, Timesmajira Online,Katavi

Mtoto mwenye umri wa miaka 14,Mkazi wa Kijiji cha Kawanzinge Wilaya ya Mpanda mkoani Katavi amefanyiwa kitendo cha ubakaji na mfungwa mmoja wa Gereza la Kalilankulukulu Wilaya ya Tanganyika wakati akitoka kupanda mpunga kwenye shamba la wazazi wake .

Tukio hilo limetokea jana Machi Mosi,2024 majira ya saa kumi na moja jioni huko katika maeneo yanayopakana na mbunga za Gereza la Kalilankulukulu ambalo ni maarufu kwa kilimo cha Mpunga.

Imedaiwa kuwa kabla ya kufanya tukio hilo mtuhumiwa huyo ambaye ni mfungwa aliwateka watoto wenzake na muathitika wa kitendo hicho cha ubakaji waliokuwa nae.

Kisha aliwatishia na ndipo alipomchukua mtoto huyo na kumpeleka kwenye kichaka na kumfanyia kitendo hicho cha kumbaka mpaka alipo maliza haja yake.

Inadaiwa kuwa mfungwa huyo kabla ya kutenda kosa hilo alikuwa akichunga ng’ombe katika eneo ambalo msichana huyo akiwa na wenzake walikuwa wakitembea kwa miguu wakati wakitoka shambani.

Mwenyekiti wa Kijiji hicho cha Kawanzinge Emanuel Machela amesema kuwa yeye alipata taarifa siku hiyo ya tukio majira ya saa tatu usiku kuwa kuna mtoto ambaye ni mwananchi wake amebakwa na mfungwa mmoja wa Gereza la Kalilankulukulu wakati akitoka shambani kupanda mpunga.

Amesema baada ya kupata taarifa hizo alimpiga simu Mkuu wa Gereza hilo msaidizi wake alimweleza kuwa ni kweli wananchi wa kijiji chake walikwenda kwenye gereza hilo na kutoa taarifa kuwa mtoto huyo amebakwa hata hivyo aliwaruhusu warudi kijijini kwa sababu walikuwa hawajathibitisha kama amebakwa.

“Baada ya kufika kijijini hapa wakiwa na kijana mmoja jina tunalo aliyekuwa na binti huyo,katika maelezo yake alisema walipokuwa kwenye gereza hilo na walipo toa taarifa mtoto huyo alipimwa kwenye zahanati ya gereza hilo na kuonekana amebakwa na kupewa dawa,”.

Muathirika wa kitendo hicho cha ubakaji kinachodaiwa kufanywa na mfungwa huyo ameeleza kuwa kabla ya kufanyiwa kitendo hicho mtuhumiwa huyo alimpinga gwala na kisha alimfunga na sweta aliyokuwa nalo usoni na kuanza kutekeleza Nia yake ya kumbaka licha ya kupiga kelele lakini hakujali.

“Alipomaliza kunifanyia unyama huo aliniuliza mtoto na kiasi gani cha fedha ili aweze kuniachia,nilimwambia kuwa Nina kiasi cha shilingi elfu mbili ambazo alizichukua,”.

Baba mzazi wa mtoto huyo jina limehifadhiwa amesema kuwa mtoto wake huwa anakawaida ya kwenda kufanya vibarua kwenye mbuga za mpunga,uwa anaondoka asubuhi na kurudi jioni lakini siku hiyo hakuweza kurudi mapema hadi saa tatu usiku na kupata mashaka yeye na mkewe hali ambayo iliwafanya waende wakawatafute watoto wenzake waliondoka nae.

Baada ya kuwafuata watoto hao mmoja wao aliwaambia kuwa mwenzao amebakwa na mfungwa hali iliomlazimu kutoa taarifa kwa Mwenyekiti wa Kijiji ambae alimpigia msimu Kaimu Mkuu wa Gereza ambaye alimjibu kuwa malalamiko ya kubakwa kwa mtoto huyo yamekishwa gerezani hapo.

“Tukiwa tumekaa kwa muda mrefu mtoto wangu alifika hapo kwa mwenyekiti na alieleza jinsi alivyo bakwa ndipo tuliamua kutoa taarifa kwenye kituo cha Polisi cha Kata ya Kakese ambako walituambia twende moja kwa moja kwenye kituo cha Polisi cha Wilaya ya Mpanda na kisha tulimpeleka hospitali ya Manispaa ya Mpanda,”ameeleza Baba wa mtoto huyo.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Dkt.Limbu Mazoya amethibitisha kumpokea mtoto huyo kwenye hospitali ya Manispaa ambapo baada ya kufanyiwa uchunguzi imethibitika kuwa mtoto huyo amebakwa.

Kaimu Mkuu wa Gereza la Kalilankulukulu analiyetambulika kwa jina moja la Bosco amesema kuwa yeye hana mamlaka ya kuzungumzia suala hilo hadi Mkuu wa Gereza alitolee ufafanuzi.

Kamada wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Katavi,Kaster Ngonyani baada ya kupigiwa simu amesema kuwa hana taarifa na tukio hilo kutokea huku akiahidi kulifuatilia licha ya kuwa tukio hilo limetokea Februari 29 mwaka huu na muathirika kupewa PF3 na jeshi hilo.