Na Heri Shaaban,Timesmajiraonline,Dar
IMEELEZWA kuwa mwaka 2030 ajira zitaongezeka kwa vijana kutokana na matumizi ya mfumo wa TEHAMA.
Hayo yamesemwa jijini hapa leo Mei 31,2025 na Mkurugenzi wa Shirika la Mawasiliano Duniani Kanda ya Afrika, Dkt.Emanuel Manasseh katika mkutano 14 wa mtandao wa nchi za Afrika .
Dkt.Manasseh amesema kutokana na kukua kwa matumizi ya Intaneti kutasadia kuongezeka kwa ajira Tanzania na Afrika kwa ujumla.
Kutokana na hayo ametoa wito kwa jamii kuandaa vijana wenye ujuzi zaidi ili waweze kusaidia serikali zao katika kukuza uchumi kupitia mfumo wa TEHAMA.
“Mwezi uliopita nilikuwa Kenya katika mashindano yanayohusiana na Intaneti katika vijana kumi walioshinda vijana watano wametoka Tanzania hii inaonesha ni jinsi gani vijana wa hapa wapo vizuri katika matumizi ya TEHAMA,”amesema.
Hata hivyo amesema kuwa vijana wengi wanahitaji msaada wa mwongozo hivyo wanatakiwa watumiwe katika kutengeza vijana ili Afrika isonge mbele.
“Tusibaki nyuma hasa sekta hii ya mawasiliano ya Intaneti kwasababu ni huduma muhimu kwa kuwa vijana wanatakiwa kusikilizwa na kuongozwa katika nafasi ya uongozi na Tanzania isibaki nyuma na Dunia itambue Tanzania pia kuna vijana wa sekta ya mawasiliano ni uchumi mkubwa kupitia simu janja,”amesema Dkt.Manasseh.
More Stories
CCM kusimamia kitabu cha Hayati Songambele kiingie mtaani
Mwendokasi kuendeshwa na ENG kwa miaka 12
Vitongoji 284 Arumeru Mashariki vyafikiwa na umeme