December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya Kumbilamoto azindua kampeni ya usafi

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salam Omary Kumbilamoto amezindua kampeni ya Usafi Wilaya Ilala iliyoandaliwa na Kampuni ya Udalali AMAZ AUCTION MART .

Uzinduzi huo wa kampeni endelevu safisha Jiji la Dar es Salaam ulizinduliwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Wilaya ya Ilala ulienda sambamba kutoa zawadi za mwaka mpya kwa Wamama waliojifungua leo hospital ya Mnazi Mmoja .

Akizindua Kampeni hiyo Meya Kumbilamoto alipongeza AMAZ AUCTION MART kwa juhudi zao za kuunga mkono kampeni endelevu ya Usafi ambayo ilizinduliwa mkoa Dar es Salaam.

“Nampongeza Mkurugenzi wa AMAZ Auction Mart Dawa Jumanne kufanikisha uzinduzi huu wa Usafi leo sambamba na kutembelea wagonjwa. Hospitali ya Mnazi Mmoja na kutoa misaada mbalimbali kwa Watoto na wamama waliojifungua” alisema Kumbilamoto

Meya Kumbilamoto aliwataka wananchi wa Wilaya Ilala kutekeleza agizo la Usafi kwa kufanya Usafi katika maeneo yao kila wakati sambamba na kuwataka wananchi kuifadhi taka katika vifaa maalum.

Alisema Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam imeshazindua kampeni ya Usafi leo wanafanya Usafi na AMAZ AUCTION MART ni mwendelezo kuhakikisha Wilaya Ilala inakuwa safi kila wakati katika mitaa yake.

Meya Kumbilamoto aliwataka wananchi kufuata taratibu za usafi ikiwemo kutunza mazingira katika maeneo yao .

Mkurugenzi wa AMAZ Auction Mart Dawa Jumanne alisema anaunga mkono Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kufanya usafi ili Wilaya ya ILALA na Dar es Salaam ipendeze.

Dawa Jumanne alisema Kampeni hiyo ya usafi ni endelevu katika Wilaya Ilala watakuwa wanafanya maeneo mbalimbali pamoja na shughuli za kijamii katika kuisaidia Serikali kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.