December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya Kumbilamoto awataka Maafisa Ustawi kufatilia watoto wenye mahitaji maalum

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MEYA wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amewataka Maafisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri hiyo kufatilia watoto wenye mahitaji maalum ambao hawajaenda shule kwa ajili ya Ulemavu ili wafamike wapatiwe Baskeli maalumu ya miguu miwili itakayowaezesha kuitumia kwenda shule

Meya Kumbilamoto alisema hayo alipokuwa akikabidhi Baskeli ya magurudumu mawili , kata ya Jangwani katika familia ya Abrahaman ambaye mtoto wake ana ulemavu wa miguu alikuwa awezi kutembea .

Meya Kumbilamoto aliwataka wananchi wa Wilaya Ilala ambao wana watoto wenye mahitaji maalum wanashindwa kusoma watoe Taarifa ofisi ya Meya waweze kupewa baskeli aina hiyo waweze kuwasaidia kwenda shule kusoma.

Naagiza maafisa Ustawi wote kufatilia taarifa za watoto wenye mahitaji Maalum ambao wapo nyumbani watambulike waweze kupewa Baskeli waende shule kusoma .

Aidha Meya Kumbilamoto ameagiza Afisa Ustawi kufatilia familia ya Abrahaman aliyopewa Baskeli aweze kupelekwa shule aanze kusoma

Diwani wa Jangwani Zakharia Digosi amempongeza Meya Kumbilamoto kwa jitihada zake za kusaidia Jamii mbalimbali ikiwemo watoto wa makundi maalum.