December 24, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya Kumbilamoto apeleka madaktari bingwa Vingunguti

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Meya wa halmashauri ya Jiji Omary Kumbilamoto amepeleka MADAKTARI BINGWA wa kituo Cha Tiba Cha magonjwa Mbalimbali kutoka DSB Polyclinic ya Dar es Salaam kwa ajili ya kumchunguza Afya Mwananchi wake wake wa Kata ya Vingunguti Ally Salum, ambaye kwa muda wa miezi mitano yupo ndani bila matibabu yoyote.

Meya Kumbilamoto afika na madaktari Bingwa wa DSB Polcinic Leo Kata ya Vingunguti ambapo walimfanyia vipimo mbalimbali Salum Ally baada kukosa matibabu kwa muda wa miezi mitano kutokana na kukosa pesa za matibabu .

“Leo nimefika nyumbani kwa Ally Salum kwa ajili ya kupatiwa matibabu baada madaktari kumfanyia uchunguzi wa Afya yake tunamuombea Mwezetu Afya yake uweze kuimalika “alisema Kumbilamoto .

Meya Kumbilamoto alisema Wananchi wa Wilaya ya Ilala ni muhimu kuwa na Bima ya Afya kwa ajili ya matibabu mbali mbali kuangalia Afya zao ” alisema Kumbilamoto .

Meya Kumbilamoto alimpongeza madaktati wa Polclinic kufuata wananchi kutoa huduma za afya katika kuunga mkono Serikali kufuata wagonjwa .

Mke wa Ally Salum ,Zulfa Salehe alisema matatizo ya mumewe yalianza mwaka jana Mwezi septemba toka wakati huo mpaka Sasa alikuwa anaugulia ndani ajawai kufika Kituo Cha afya .

Muuguzi Mkunga kutoka DSB Polyclinic Issa Mmbaga alisema Polyclinic imemkatia Bima ya Afya ya NHIF Mke wa Ally Salum ,Zulfa Salehe Ili akipata matatizo aweze kupata matibabu ya haraka.

Muuguzi Mkunga Issa Mmbaga alisema Mgonjwa Ally Salum amepewa matibabu Bure kutoka kituo Cha Tiba ya magonjwa Mbalimbali DSB kilichopo Wilayani Ilala .

Mmbaga alisema maradhi mengi kwa Sasa lwa Jamii maradhi yasio ambukiza serikali inawataka Wananchi muhimu kuwa na Bima ya Afya kupata huduma za haraka .