December 28, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya Kumbilamoto akabidhi mabomba ya DAWASA liwiti

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online

MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto amekabidhi mabomba ya maji safi na Salama kwa ajili ya wananchi wa kata ya Liwiti ambao Mabomba yao ya DAWASA yalikatwa na GREDA wakati wa kuchonga barabara mtaa Misewe LIWITI Wilaya Ilala.

Kufuatia kukatika mabomba hayo ya Mtaa kero hiyo Diwani wa Liwiti Alice Mwangomo ,aliwasilisha kwa Meya Kumbilamoto ambapo leo Meya ametatua kero hiyo kwa kugawa mabomba ili DAWASA waweze kuwaunganishia wananchi wa misewe.

Akizungumza mara baada kukabidhi mabomba hayo Meya Kumbilamoto aliagiza kila uongozi wa Kata watoe sheria kali miundombinu ya DAWASA iwe ina pita chini mabomba yasiwe yanakatwa kila wakati wakati wa kuchonga barabara.

“Naagiza uongozi wa kila kata ndani ya Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam kuweka sheria DAWASA wawe wanafukia mabomba chini ili yasiingiliane wakati wa kujenga Barabara sababu mabomba yanapokatwa upelekea wananchi kukosa maji “alisema Kumbilamoto.

Meya Kumbilamoto alimshukuru mdau wa maendeleo aliyemsaidia kutatua kero za wananchi na kumpatia mabomba ya shilingi milioni 1.5 Ambapo aliwataka DAWASA Wilaya ya TABATA kufunga haraka ili Wananchi waweze kupata maji safi na salama.

Wakati huo huo Meya Kumbilamoto alizungumzia ujenzi wa barabara za Halmashauri ambapo alisema Serikali imeshatenga pesa za kutosha kwa ajili ya kujenga Barabara za Halmashauri pia Halmashauri imetoa vijiko vitatu kwa ajili kukarabati barabara za Wilaya ya Ilala zote greda litapita kila kata kwa ajili ya matengezo.

Katika hatua nyingine Meya Kumbilamoto alizungumzia Mikopo ya Serikali ambayo inatoletolewa ngazi ya Halmashauri Serikali ya awamu ya sita ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan imetenga shilingi bilioni 8 za mikopo amemwagiza Diwani wa Liwiti kusimamia wananchi wake wawezeshwe Mikopo ya Serikali.

Diwani wa Kata ya Liwiti Alice Mwangomo alimpongeza Meya Kumbilamoto kwa kutatua kero hiyo ya mabomba ya maji ya DAWASA ambayo yalikatwa.

Diwani Alice Mwangomo alitoa kero nyingine kwa Serikali akitaka wananchi wake vyoo vyao viunganishwe na mfumo wa maji taka ili kuondoa changamoto zinazowakabili ikiwemo kukamatwa kila wakati na watu wa mazingira kutokana na mfumo wa maji taka Kata ya Liwiti amna na makazi ya eneo hilo yapo eneo la maji kila wakati vyoo vinajaa