November 5, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya awataka wazazi kulinda watoto

Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala

Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Omary Kimbilamoto, amewataka wazazi Wilayani Ilala kila mmoja kumlinda mtoto wake Ili asiingie katika vitendo vya mmomonyoko wa maadili .

Meya Kumbilamoto, alisema hayo wilayani Ilala wakati wa kuzungumza na wazazi na Wanafunzi wa shule ya Msingi Vingunguti wakati alipokuwa akipokea msaada wa Madawati kutoka kwa wadau wa sekta ya Elimu Tanga Pharmacetical Plastics Ltd.

“Wazazi wangu walezi wa watoto naomba kila mmoja awe Mlezi wa mtoto wake kuhusiana na vitendo vya mmomonyoko wa maadili Vingunguti Ukatili wa Kijinsia inauhusika maadili sio mazuri Mtaani ” alisema KUMBILAMOTO

Meya Kumbilamoto aliwataka Wazazi Wilayani Ilala kufuata miongozo ya Dini na kukemea Maswala ya kikatili kwa Jamii ya Taifa la nchi yetu .

Akizungumzia Sekta Elimu Meya KUMBILAMOTO alipongeza wadau wa Tanga Pharmacetical Plastics kwa msaada wa madawati kwa ajili ya shule hiyo ambapo aliwataka Wadau wengine kuunga mkono sekta ya Elimu Juhudi za kuisaidia Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan .

Meya KUMBILAMOTO alitoa cheti cha utambuzi kwa kutambua mchango wa Tanga Pharmacetical Ltd katika sekta ya Elimu wamekuwa wakisaidia Shughuli mbalimbali za kijamii .

Alisema awali walishatoa friji Saba za maji ya kunywa shule zote Wanafunzi wanakunywa maji safi na Salama .

Akizungumzia shule hiyo kitaaluma Meya KUMBILAMOTO alisema shule hiyo kila mwaka inafanya Vizuri mwaka 2022 wameferi Wanafunzi watano.

Mlezi wa Vingunguti Batuly Mziya alimpongeza Meya Kumbilamoto anafanya kazi kubwa katika kupambania Jamii ambapo katika kata ya Vingunguti ameboresha sekta ya Afya Zahanati ya Vingunguti Pamoja na kuwakabidhi gari ya wagonjwa Ambulance .

DIWANI Batuly Mziya alisema Meya Kumbilamoto pia anakisaidia vizuri chama Cha Mapinduzi CCM Mwaka 2025 anatosha kuwa Diwani kuongoza Wananchi wake .

Meneja Mwajili wa Tanga Pharmaceutical
Plastics ltd Stephen Godfrey alisema Kampuni yao Makao Makuu Tanga ,Dar es Salaam Ofisi zipo Vingunguti pia wanajishughukisha na Vipodozi akimpongeza MEYA Kwa kumpa Ushirikiano .