January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa

Na Ashura Jumapili TimesMajira online Bukoba,

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba , ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nshambya Godson Gibson,amewaandalia mafunzo wenyeviti wa mitaa na wajumbe wa kata yake yanayohusu wajibu na majukumu yao ya kiutendaji.

Gibson,amesema kikichomsukuma kutoa mafunzo hayo ni kutokana na Rais wa awamu ya 6 Dk.Samia Suluhu Hassan anavyotoa elimu kwa watu mbalimbali.

Amesema aliwahaidi viongozi mbalimbali wa Kata hiyo kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa kuwa atawapa semina ya mafunzo ya kujua majukumu na wajibu wao katika nafasi zao za kuwatumikia wananchi.

Amesema viongozi hao wamejifunza mada sita zitakazo wasaidia katika utekelezaji wao wa majukumu kwenye maeneo yao.

Mbali na mafunzo hayo Diwani huyo ameamua kutoa vitendea kazi kwa wenyeviti wa mitaa mitatu ya Kata ya Nshambya ambavyo ni limu boksi 2 na karamu 100 kila mtaa na hiyo ni muendlezo .

Anna Mshumbusi ni mjumbe wa mtaa wa Bunkango anasema mafunzo hayo yamewajenga na yatawasaidia katika shughuli zao za kuwapngoza wananchi.

Msumbusi,anasema hawatamuangusha Diwani wao kwa mafunzo aliyowapa katika kutekeleza majukumu yao.

Hata hivyo amesema zipo changamoto nyingi katika uongozi hasa baadhi ya wananchi kutokuwa na uelewa wa kutosha kuhusu masuala ya kisheria.

Athuman Ibrahim ambaye alikuwa mtoa mafunzo ambaye pia ni mtendaji wa Mtaa wa migera ,aliwafundisha wenyeviti hao na wajumbe juu ya uwanzishwaji wa serikali za mitaa sababu na Asili yake.

Ibrahim anasema kuwa lengo la kuanzishwa kwa mamlaka za serikali za mitaa ni kusogeza huduma karibu kwa wananchi na uwakilishi wa moja kwa moja .

Anasema serikali za mitaa zinaumuhimu mkubwa katika maendeleo ya jamii na hutoaji wa huduma kwa wananchi.

Anasema wenyeviti wa mitaa na wajumbe wapo chini ya mamlaka za serikali za mitaa na lengo mahususi ni kukuza ushiriki wa Wananchi katika maamuzi na kwakuwa zipo karibu na wananchi zinawezesha kushiriki kikamilifu kusimamia rasilimali za kijamii kwa ufanisi.

Anasema viongozi wa serikali za mitaa wanawajibu wa kusimamia na kugawa rasilimali za kijamii kwa namna inayofaa ili kuhakikisha wananchi wote wananufaika.

Anasema,Asili yake ni kutokana na kuwa na mfumo wa usimamizi unaoweza kufikia wananchi moja kwa moja badala ya kutegemea serikali kuu.

Anasema mfumo huo ulianza kwa nchi nyingi baada ya kuona umuhimu wa kuwa na ngazi ya chini ya serikali inayoweza kutoa huduma kwa haraka na ufanisi.

Anasema cheo cha mwenyekiti wa mtaa Tanzania kilihasisiwa kupitia mfuno wa serikali za mitaa ulioundwa rasmi baada ya uhuru wa Tanganyika mwaka 1961 na baada ya kuasisiwa ziliimarishwa zaidi na mabadiliko ya kiutawala yaliyofanyika mwaka 1970 na 1980.

Anasema cheo hicho kikianzishwa kwaajili ya kuleta karibu zaidi huduma za kiutawala kwa wananchi ngazi ya chini ya jamii.

Anasema miongoni mwa shughuli za wenyeviti wa mitaa ni pamoja na kuhakikisha rasimali zinazoanxishwa katika ngazi ya mtaa zinawafikia wananchi moja kwa moja na kuwanufaisha.

Anasema kwa mujibu wa sheria za serikali za mitaa imegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni sheria ya serikali za mitaa sura namba 288 inahusu mijini na sheria ya serikali za mitaa vijijni sura namba 287.

Kwa upande wake mgeni rasmi katika mafunzo hayo katibu tawala wilaya ya Bukoba ( DAS )Proscovia Jaka mwambi,amesema kitendo cha diwani wa Kata ya Nshambya cha kugharamia mafunzo ya uongozi ya wenyeviti wa mitaa na wajumbe ni cha upendo wa hali ya juu.

“Sio viongozi wote wanaweza kufanya jambo hili mmebarikiwa ,muendelee kufanya naye kazi kama kuna changamoto yoyote muelezeni maana hakuna binadamu mkamilifu na sio kuongelea pembeni”anasema Jakamwambi.

Anasema wenyeviti hao wafuate kile walichojifunza maana wamepewa elimu ya kutosha kutoka kwa viongozi mbalimbali kuhusu wajibu wao katika shughuli mbalimbali za maendeleo ya mitaa yao .

Amesema kila kiongozi atambue mipaka yake wasiingulie kwenye majukumu ya kiutendaji kwa kufanya hivyo watagombana na kusababisha mgogoro.

Amewataka kuwa waaminifu na waadilifu kwa kuwa wazalendo na kusimamia misingi ya kiutawala kwa kuzingatia taratibu za kisheria sanjari na kuichukia rushwa.

Amesema ni vyema wenyeviti hao wakatenga siku katika mitaa yao ya kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua kwa wakati

Amesema viongozi hao wamatakiwa kuelewa mipaka yao wasivamie majukumu yasiyokuwa yao na amewashauri kupokewa ushauri na kuuchuja kwa maslahi mapama ya wananchi na serikali ,wasiwe viongozi wabinafsi wasio tambua wajibu wao.