Na Heri Shabani ,Ilala
MEYA wa Halmashauri ya jiji la Dar es Salaam Omary Kumbilamoto ambaye ni Diwani wa kata ya Vingunguti wilayani Ilala amekabidhi TV pamoja na kingamuzi cha AZAM kwa mashabiki wa Yanga Tawi la Kichangachui Vingunguti wilayani Ilala.
Akikabidhi msaada huo Meya Kumbilamoto aliwataka wana Yanga wa tawi la Kichangachui kukata kadi za klabu hiyo ili iweze kupata mapato ya kujiendesha na kukuza mapato ndani ya clabu yao.
“Simba na Yanga changamoto wanachama wao wanashindwa kununua kadi za klabu zao mimi meya wenu nitachangia kuwanunulia kadi za wanachama “alisema Kumbilamoto.
Aidha aliwataka wanachama wa klabu hiyo kujenga umoja na mshikamano katika kushirikiana na kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan katika sekta ya michezo,sekta ya afya na sekta ya Elimu Dkt samia amefanya mambo makubwa.
Alisema dhumuni la kuwapa TV na kingamuzi wanachama wa clabu ya Yanga Tawi la Kichangachui lililopo Vingunguti wilayani Ilala wawe wanafatilia taarifa za michezo katika klabu zao na kuangalia taarifa ya habari .
More Stories
Wananchi Ikungi watakiwa kutumia mtandao kwa manufaa
UWT yalaani shambulio la kudhuru mwili Mwenezi BAWACHA
JAB :Kazi ya ukamilishaji wa mfumo wa kidigitali wa usajili wa waandishi wa habari inaendelea