RIO DE JANEIRO, Brazil
TIMU ya taifa ya Argentina imetwaa taji la Copa America baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Brazil katika mchezo wa fainali uliochezwa usiku wa kuamkia kwenye dimba la Maracana nchini Brazil.
Katika mchezo huo goli la Argentina lilitiwa kimiani na Angel Di Maria dk 22, ambalo lilidumu mpaka dakika ya 90.
Kufuatia ushindi huo, hatimaye nyota wa Argentina anayekipiga katika klabu ya Barcelona Lionel Messi amefanikiwa kunyakuwa Kombe lake la kwanza na Timu ya Taifa.
Messi amefanikiwa kucheza fainali nne za Copa America 2007, 2015 na 2016 zote Argentina alipoteza kabla ya fainali ya nne leo kuandika historia mpya.
Mshambuliaji huyo, amefanikiwa pia kuibuka mchezaji bora wa mashindano hayo, mfungaji bora akiwa na magoli 4 na assist 5, amechangia katika magoli 9 ya Argentina kati ya 12 yaliofungwa katika michuano hii huku akicheza dakika zote 630 za michuano hiyo sawa na mechi 7.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania