December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meja Jenerali Mabele:Tanzania mahali sahihi kwa uwekezaji

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajab Mabele kutokana na mazingira ya uwekezaji kuboreshwa ,kumeifanya Tanzania kuwa mahali  salama pa kufanya biashara na uwekezaji.

Akizungumza leo Julai 3 ,2024 na waandishi wa habari katika banda la JKT kwenye maonesho ya 48 ya Kimataifa ya Biashara ,Meja Jenerali Mabele amesema   hali hiyo imefanya watu wengi zaidi kuja kuwekeza hapa nchini.

“Naipongeza Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuweka mazingira ya mazuri ya kufanya biashara na hivyo watu wengi zaidi kuja kuwekeza hapa nchini na hivyo kuifanya Tanzania kuwa mahali sahihi pa kufanya biashara na uwekezaji.

Kuhusu ushiriki wao katika amaonesho hayo ,Meja Jenerali Mabele ambaye pia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Shirika la uzalishaji Mali la JKT  (SUMAJKT) amesema  wameshashiriki maonesho hayo mara nyingi na kwamba wamekuwa wakija na bidhaa bora ili wananchi wananchi waweze kununua.

Pia amesema SUMAJKT ina  kampuni bora ya ulinzi ambayo ni miongoni mwa kampuni bora za ulinzi na ni kampuni ya watanzania ambayo ina walinzi zaidi ya 16000 katika maeneo mbalimbali

“Kwa hiyo katika eneo hilo tu tumechangia kupunguza ombwe la ajira nchini ,pia tunayo kampuni ya usafi kwa sababu kama nilivyosema tunaangalia fursa,tumeona kuna fursa katika eneo hilo watanzania wanahitaji majiji,miji yao iwe safi lakini tunahitaji lakini kuna vijana wa kitanzania ambao tumewaajiri na wapo katika kampuni ile ili kuwawezesha kutunza familia zao kwa hiyo niseme tu kwamba kampuni zetu tunazozianzisha kutokanana fursa tunazoziona na kwamba tunaweza kufanya biashara na kutoa huduma katika nchi yetu,”amesema na kuongeza kuwa

“Maonesho haya sisi tunafanya biashara ambayo husaidia kuongeza uchumi wa nchi, na mwezi  wa sita mwaka huu ,tumeshiriki katika kutoa gawio kwa hiyo ni wachangiaji katika mfuko mkuu wa Serikali, tunalipa kodi ,tena ni walipa kodi wazuri katika nchi yetu,hivi vifaa vyote  mnavyoviona hapa tunalipa kodi na hili ni jambo la msingi sana.

Kuhusu ushiriki wao wa  maonesho katika nchi nyingine amesema,wamekuwa wakishiriki maonesho hadi ya nje ya nchi na wameshaenda kwenye maonesho Commoro  ambapo wakati mwingine watu wa Comoro wanakuja kuzifuata Dar es Saaam .

Ametumia nafasi hiyo kuwahamasisha  watanzania kufika katika banda la JKT kuona na kununua bishaa zao kwani ni bidhaa bora.

Kwa upande wake Mkuu wa Tawi la Utawala rigedia Jenerali Hassan Mabena Mkuu wa Tawi la Utawala JKT amesema ,JKT limekuwa likifanya shughuli za uzalishaji mali katika Nyanja za kilimo , uvuvi na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali kupitia shirika lao la SUMAJKT.

“Kwa kuwa JKT limekuwa likichukua vijana wale wa kujitolea na wale wa mujibu wa sheria,pamoja na kufundishwa masomo ya ukakamavu ,uzalendo na hali ya kulipenda Taifa lao lakini vile vile wamekuwa wakifudishwa katika Nyanja za uzalishaji mali,

‘Sasa katika eneo hilo vijana wamefundishwa kuzalisha bidhaa mbalimbali na kupitia vikosi na shirika lao vijana hao wameweza kutumia maeneo hayo ama shamba darasa ili kuwapatia ujuzi ambao unakwenda kuwasaidia kujitafutia kipato pindi watakaporudi uraiani baada ya kumaliza mkataba wao JKT.

Aidha amesema wa upande wa SUMAJKT lina kampuni zake tanzu ambapo kuna kampuni kwa ajili ya kutengeneza bidhaa za ngozi  kwa maana ya viatu,mikoba na vitu vingine vinavyotokana na bidhaa hiyo ambapo vijana wa JKT wameonesha umahiri mkubwa na wataalam waliobobea kwwnye utengenezaji wa bidhaa hizo.

Vile Vile Brigedia Jenerali Mabena amesema pia wana kiwanda cha samani ambacho kipo Chang’ombe Dar es Salaam , vijana hao wamekuwa wakifundishwa pale kwa nadharia na vitendo huku akisema hata bidhaa ambazo zipo katika maonesho hayo ,vijana pia wameshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kila hatua.

Pia amesema wana kiwanda cha nguo ambacho kipo Mgulani ambapo vijana hao mbali na kupewa mafunzo ya JKT pia wamekuwa wakihusishwa kufundishwa kushona zile nguo hali ambayo mara baada ya kumaliza mkataba wao ule ujuzi unakwenda kuwasaidia kwenda kujitegemea.

Kuhusu changamoto ya mitaji amesema wanawafundisha katika ujasiriamali mdogo mdogo ambao wao wanaweza wakamudu na wazazi wao .

“Mfano mazao ya mshambani ,mabaki yake wakati mwingine hutumika kutengeneza sabuni,mafuta na vitu vingine,sasa vijana hawa wanafundishwa kutengeneza sabuni ambapo mtu akiwa na mtaji wa shilingi 300,000 inamtosha kununua malighafi ya kutengenezea biidhaa hiyo na hivyo kujikwamua kiuchumi,

“Kwa hiyo tunashukuru kwa uwepo wa maonesho haya kwani yamekua yakichangia katika kuwafundisha vijana kwa nadharia na vitendo.”