January 23, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Meja Jenerali Mabele:Vijana jiepusheni na matumizi ya dawa za kulevya

Na Mwandishi Wetu,Timesmajira online,Musoma

MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa Meja Jenerali Rajabu Mabele ameishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuliwezesha Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kuendesha Mafunzo ya Vijana wa Kitanzania na kuwapa stadi zitakazowasaidia katika maisha.

Meja Jenerali Mabele ameyasema hayo leo Machi 17,2023 wakati akihitimisha Mafunzo  ya Awali ya Kijeshi  kwa Vijana wa Kujitolea Operesheni Jenerali Venance Mabeyo  katika kikosi cha Rwamkoma JKT mkoani Mara.

Sanjari na Hilo, Amewasihi Vijana hao kutunza afya zao pamoja na kujiepusha na matumizi ya Madawa ya kulevya .

Naye Mkuu wa Jeshi la Kujenga Uchumi Zanzibar  (JKU) Kanali Makame Daima amewapongeza Vijana hao kwa kuhitimu mafunzo yao na kuwataka kwenda kukiishi kiapo chao.

Akimkaribisha Mkuu wa JKT kutoa nasaha na kufunga mafunzo hayo, Mkuu wa Tawi la Mafunzo JKT Kanali Aisha Matanza amesema, Vijana hao wamewawakilisha Vijana wenzao katika makambi yote yaliyoendesha Mafunzo hayo.

Akitoa taarifa ya Mafunzo, Kamanda Kikosi cha Rwamkoma JKT, Luteni Kanali Gaudencia Mapunda amesema.Vijana wa Kujitolea Operesheni Jenerali Venance Mabeyo yalifunguliwa Novemba 28, 2022 katika Makambi ya JKT yaliyoendesha Mafunzo hayo yalliyochukua majuma 16.

Aidha amesema ,mafunzo hayo  yalianza kuhitimishwa kwa tarehe tofauti kuanzia Machi 7, 2023 hadi leo hii Machi 17,2023 Mkuu wa JKT amefunga zoezi la uhitimishwaji wa mafunzo hayo.