Na Heri Shaaban, TimesMajira, Online
MBUNGE wa Jimbo la Ilala ambaye ni Naibu Spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu, amesema mikakati yake katika Jimbo la Ilala kuanzisha Jukwaa la uwezeshaji Wananchi kiuchumi ili liweze kuwasaidia wanawake fursa mbali mbali za kiuchumi.
Mbunge Zungu alisema hayo kata ya Gereza Kariakoo wilayani Ilala, alipokuwa akizindua Jukwaa la nne la Jimbo la Ilala ambapo aliwataka wanawake wa Gerezani kujenga umoja na kupendana waache kusemana katika vikundi.
“Leo tumezindua Jukwaa la Uwezeshaji Wananchi kiuchumi jukwaa la nne katika jimbo la Ilala kuzinduliwa na kesho (yani leo )tunazindua jukwaa la tano la wanawake katika kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan majukwaa haya yaweze kusaidia fursa za wanawake mimi Mbunge wenu mikakati yangu kuanzisha jukwaa la jimbo litakalo wasaidia wanawake wote”alisema Zungu
Mbunge Mussa Zungu aliwataka Wanawake wa Jimbo la Ilala kufanya biashara kwa nidhamu wajipange vizuri kwa umoja wao na mshikamano wampe nguvu Rais Samia Suluhu Hassan kushinda kwa kishindo 2025 .
Alimwagiza Afisa Maendeleo wa Gerezani kuwapa ushirikiano Wanawake wa eneo hilo vikundi vyao viweze kusajiliwa waweze kupata mikopo ya Serikali wajenge umoja waache kusemana .
Aidha Zungu alisema Biashara ni Taaluma wanawake wamepewa elimu kubwa na Taasisi za Benki katika kuendeleza biashara zao ambapo wakitumia simu vizuri na mitandao ya kijamii watanufaika .
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake Gerezani Jamila Simba alisema jukwaa la Wanawake Gerezani litawanufasha wanawake wote waweze kujikwamua kiuchumi katika kukuza mitaji yao ya biashara waweze kupata masoko ya ndani na nje ya nchi.
Mwenyekiti Jamila Simba aliwataka wanawake kushirikiana na kutafuta fursa za kiuchumi waweze kukuza uchumi wa nchi wasaidie Serikali kukuza uchumi wanawake wenye biashara ndogo ndogo wawe wafanyabishara wakubwa.
Diwani wa Kata ya Gerezani Fatuma Abubakari, alimpongeza Mbunge Zungu kutoa elimu ya mafunzo ya ujasiriamali wanawake wa Gerezani ambapo aliwataka wanawake watumie elimu hiyo kupata masoko makubwa .
Mlezi wa Jukwaa la Wanawake Gerezani Asha Johari , aliwataka wanawake kuwa wamoja ,kujenga umoja na mshikamano huku wakifanya biashara zao ili wakuze uchumi wa nchi kujitangaza katika masoko.
More Stories
Waziri Mavunde:Benki Kuu yanunua tani 2.6 za Dhahabu nchini
Kampeni msaada wa kisheria ya mama Samia kutatua kero za kisheria Katavi
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25