Na Doreen Aloyce,TimesMajira Online, Dodoma
MBUNGE Viti Maalumu kwa kupitia chama cha Civic United Front (CUF) Mkoa wa Lindi, Riziki Lulida ameomba kurudi Chama Cha Mapinduzi (CCM) mara baada ya kumkubali Rais John Magufuli kwa uchapakazi wake.
Lulida ameomba ridhaa hiyo Bungeni Dodoma wakati alipokuwa akichangia bajeti kuu ya Serikali mwaka 2020/21. Amesema kuwa ameamua kurudi nyumbani kutokana na kuridhishwa na utendaji kazi na usikivu wa Rais Magufuli alionao kwa wananchi na taifa kwa ujumla.
“Naomba niombe ridhaa ya kurudi nyumbani kumenoga nimelelewa na CCM, Mheshimiwa Rais amekuwa msikivu nakumbuka ilikuwa mwaka 2015 alinikuta nje ya bunge akaniuliza naenda wapi nikamwambia naenda nyumbani kufuturu alinipeleka mpaka nyumbani na tukashiriki wote ilionyesha ni kiasi gani Rais wetu ni mtu wa watu na mwenye upendo” amesema Lulida.
“Natanguliza msamaha kwa wote niliowakosea na mimi nawasamehe wote walionikosea naomba mnipokee ili tuendeleze gurudumu la kumuunga mkono Rais “amesema Lulida.
More Stories
Baraza la Wafanyakazi Ofisi ya Mwanasheria Mkuu latakiwa kutoa huduma bora za kisheria
Korea yaonesha utayari kuwekeza nchini katika uendelezaji wa madini mkakati
Serikali ya Kijiji Ilungu yawakatia bima za afya wananchi 1500