November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge wa Viti Maalumu Chadema Mkoa wa Ruvuma, Yosephar Komba

Mbunge wa Chadema atolewa Bungeni

Na Doreen Aloyce, Timesmajira Online, Dodoma

MBUNGE wa Viti Maalumu Chadema Mkoa wa Ruvuma, Yosephar Komba ametolewa ndani ya Bunge kwa kile kilichoelezwa kuwa ni uvunjifu wa maadili baada ya kuwasha kipaza sauti na kuongea bila ruhusa ya Spika Job Ndugai.

Msuguano huo umetokea wakati mchango uliokuwa ukiendelea kutoka kwa Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa Ruvuma CCM juu ya bajeti pamoja na manyanyaso ya ugoni yanayotolewa na viongozi wanawake kutoka upinzani.

Awali Mbunge wa Viti Maalumu, Jackline alisema, kutokana na manyanyaso ya ugoni ambayo wamekuwa wakifanyiwa wabunge wanawake wa upinzani akiwemo mbunge huyo Yosephar Komba ambaye aliwahi kumuelezea tatizo hilo kuwa nae ni mhanga wa matatizo hayo.

“Naomba Msajili wa Vyama vya Siasa aingilie kati na ikiwezekana viondolewe kabisa ili kuacha kunyanyasa wanawake hao.”amesema

Hata hivyo ghafla Yosephar Komba alianza kupiga kelele kwa kutaka kutoa taarifa huku akiwa amewasha kipaza sauti bila kumtii Spika jambo ambalo lilimfanya Spika Ndugai kuamuru atolewe nje.