Na Heri Shaban, Timesmajira Online, Ilala
Mbunge wa Jimbo la Segerea Bonnah Ladslaus Kamoli, amefanya ziara katika jimboni humo na kuwapa pole wananchi waliokumbwa na mafuriko katika Bonde la Mto Msimbazi wilayani Ilala.
Kamoli,amefanya ziara hiyo katika Kata tano kwa ajili ya kuangalia athari za mvua ya El Nino inayoendelea kunyesha maeneo mbalimbali nchini hapa.
“Wakati mvua zinaleta athari nilikuwa katika vikao Bungeni tumemaliza nimewakimbilia kuwapa pole wananchi wangu ambao kaya zetu zimekumbwa na mafuriko katika Bonde la Mto Msimbazi,”amesema Bonnah.
Bonnah katika ziara yake leo ametembelea Kata ya Kipawa ambapo wameathirika wa mafuriko ni wananchi 94 na mvua hizo huku Kata ya Liwiti wakiwa 71 na nyumba zao zimeenda na majipi
Pia ameagiza wakazi wa Kipawa na Liwiti ambao nyumba zao zimesombwa na mafuriko wasiongeze majina hewa labda yatokee mafuriko mengine usiku wa leo badala yake idadi hiyo iliyotambulika wasubiri utaratibu wa Serikali.
Ametumia nafasi hiyo kumpongeza Mkuu wa Wilaya ya Ilala Edward Mpogolo na viongozi wa CCM wilaya hiyo wakiongozwa na Mwenyekiti wake Saidi Sidde walipofanya ziara siku ya kwanza .
Aidha amewambia wananchi wa mto Msimbazi maji sasa hivi yamekosa kwa kupita yanapita kwa wananchi ambapo alishauri Serikali kumuomba Mkandarasi aliyepewa kazi ya kujenga mto Msimbazi kuanza maeneo ya makazi ya watu ambayo yapo Bonde la Mto Msimbazi, Kalakata,Tabata,Kipawa na Mnyamani.
Katika ziara hiyo leo Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli alitembelea Tabata,Bonyokwa,Kipawa,Liwiti na Mnyamani, kuangalia athari za mafuriko na kuangalia miundombinu ya barabara.
More Stories
Kapinga atoa maagizo TANESCO ,kuhusu Vijiji vinavyolipia gharama ya mijini kuunganisha umeme
Ukiukaji wa Uhuru wa Kidini na Kutovumiliana Huzusha Malumbano ya Kimataifa
NLD kipo tayari kwa uchaguzi wa Serikali za Mitaa