January 15, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge mstaafu Mbarali Haroon Pirmohamed achukua fomu kugombea NEC Mkoa wa Mbeya

Na Esther Macha, Timesmajira,Online,Mbeya

ALIYEKUWA Mbunge mstaafu wa jimbo la Mbarali na Mwekezaji wa kampuni ya Mbarali Estate,Haroon Mulla Pirmohamed amechukua fomu ya kugombea  nafasi ujumbe wa halmashauri kuu ya taifa (NEC)kupitia mkoa wa Mbeya .

Fomu hiyo amekabidhiwa leo  na Katibu wa chama cha mapinduzi (CCM)mkoa wa mbeya ,Mwalimu Shaibu Akwilombe.

Aidha Akwilombe amesema kwa nafasi za juu za chama kwa upande wa nafasi ya Mwenyekiti wa mkoa waliochukua ni watu watatu   akiwepo Mwenyeiti wa aliyemaiza muda wake  Mchungaji Jacob Mwakasole.

 Kwa  upande wa nafasi ya halmashauri kuu Taifa  (NEC)  Mkoa wa Mbeya idadi ya walichukua fomu ni watu wanne akiwepo  Mwekezaji huyo na Mkurugenzi wa Shule za Paradise na Patrick  Mission Ndele Mwaselela,

Alibainisha kuwa kwa nafasi ya  Katibu wa siasa na uenezi    mpaka sasa   ni watu watatu akiwepo anayetetea nafasi yake  Bashiri Madodi .

Hata hivyo Katibu huyo amesema kuwa wanachama wanaendelea  kuchukua fomu kuwania nafasi mbali mbali za uongozi  ndani ya chama.