LONDON, Mbunge wa Jimbo la Peterborough Mashariki mwa England, Paul Bristow ametangaza kuwa amefunga swaumu wiki nzima ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa lengo la kuutambua vyema mwezi huu na swaumu ya wafusi wa dini ya Kiislamu duniani.
Bristow ambaye ni mbunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Conservative tangu mwaka jana ametangaza uamuzi huo katika ujumbe wake wa video kwenye mtando wa Twitter.
“Ramadhani ni wakati wa kutafakari kwa kina masuala ya kiroho, kijitakasa na kufanya ibada. Kwa juma la kwanza la Ramadhani, nami nimeamua kufunga, kujifunza zaidi juu ya huu mfungo. Mimi si Muislamu,”amesema.
Mbunge huyo wa Uingereza ameongeza kuwa, kuna umuhimu wa kushirikiana na Waislamu katika ibada hiyo muhimu.
More Stories
Wizara ya madini yakusanya bil.521 nusu ya kwanza mwaka wa fedha 2024/25
Meya awafunda wenyeviti Serikali za Mitaa
Mgeja aipongeza CCM kwa uteuzi Wagombea Urais