Na Esther Macha, Timesmajira Online, Chunya
WAUMINI wa dini ya kiislamu wilayani Chunya Mkoani Mbeya wameshikwa mkono wa Eid El Fitri na Mbunge wa Jimbo la Lupa ,Masache Kasaka ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa dini zote.
Sadaka hiyo Michele na nyama ambayo imekabidhiwa katika Msikiti wa Wilaya ya Chunya mkoani Mbeya na na Katibu wa Chama cha mapinduzi wilaya ya Chunya Charles Jokel aliyemwakilisha Mbunge wa Jimbo la Lupa Masache Kasaka.
Aidha Masache amesema lengo kuu la kuwashika mkono waislamu ni kuendelea kuungana na waumini wa dini hiyo katika kusherehekea pamoja sambamba na kusaidia wahitaji wasiojiweza.
Charles Jokel ni Katibu wa CCM wilaya ya Chunya amezungumza kwa niaba ya Mbunge amesema Mbunge Masache ametoa sadaka kwa waumini wote wa dini hiyo ili waweze kusherehekea kwa amani na utulivu na pia kumuombea Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan.
Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Chunya ,Sheikh Nurdin Jicha amempongeza Mbunge Masache kwa kuwakumbuka waumini wa kiislamu kwa kutoa sadaka yake.
Shekhe Jicha amewaomba waislam wote kuendelea kuiombea serikali ya Awamu ya sita chini ya Rais wetu Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na watendaji wake wote wa ngazi za jumapili na chini ili waweze kufanya Kazi za wananchi pasipo vikwazo.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa Â
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi