
Na Joyce Kasiki,Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Misenyi, Florent Kyombo, ameuliza Bungeni kuhusu lini Serikali itaanza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kyabajwa uliopo Mkoa wa Kagera.
“Je ni lini Serikali itaanza ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kyabajwa uliopo Mkoa wa Kagera.?”amehoji Kyombo
Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Uchukuzi alisema kuwa Serikali tayari imeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa Kiwanja kipya cha Ndege cha Mkoa wa Kagera .
Alisema Tayari serikali imeshaingia mkataba na Mtaalamu Elekezi kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa mradi huo.
Kihenzile amesema kuwa, kiwanja hicho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Kyabajwa.
Kwa.mujibu wa Naibu Waziri huyo, Mtaalamu Elekezi anatarajiwa kukabidhiwa eneo la kazi na kuanza majukumu yake ndani ya robo ya tatu ya mwaka wa fedha 2025/2026, ambayo ni kati ya Januari hadi Machi, 2026.
Aidha, alisema kuwa ,kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina imepangwa kukamilika mwishoni mwa mwaka 2026.
Amesema , baada ya hapo hatua za utekelezaji wa ujenzi wa mradi huo zitaanza rasmi.

More Stories
Kihongosi amtaka mkandarasi kuwalipa vibarua stahiki zao
DC Mbozi afuturisha wananchi, asisitiza mshikamano na Umoja.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali: Nina imani mubna utendaji kazi wa ofisi ya Mwandishi Mkuu wa Sheria