Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online, Iringa
Wito umetolewa kwa Wanawake wote nchini, kushikamana kwa kuhakikisha wanamuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika jitihada zake mbalimbali za kuwainua wanawake kiuchumi.
Wito huo umetolewa na Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Rita Kabati wakati wa kongamano la wanawake wa Mkoa wa Iringa aliloliandaa hivi karibuni kwa kushirikiana na Kanisa la KKKT Dayosisi ya Iringa, lililolenga kuwajengea uwezo wakina mama wa mkoa huo katika masuala mbalimbali ya kisiasa na kiuchumi.
Amesema ni wazi kuwa katika uongozi wa Rais Samia, wanawake wa Tanzania wameendelea kuimarika siku hadi siku katika nyanja mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupata nafasi za uongozi Serikalini, na kwamba wanawake wanapaswa kushikamana na kumuunga mkono Rais Samia kwa kuchapa kazi ili kuleta tija katika Taifa.
“Kwa Sasa tunaona wanawake wengi wanapambana katika kijikwamua kiuchumi na ndio maana hatuteteleki katika kufanya kazi. hivyo ni wajibu wetu kama wanawake kufanya juhudi za kuongeza kipato” amesema.
Akizungumzia Mikopo ya Halmashauri ambayo kwa sasa imesimamishwa kwa muda ili kufanya maboresho, amesema wanawake wanapaswa kuwa waaminifu kwa kuanzisha vikundi vyenye weledi mkubwa, na kuwa wa kweli, ili kuisaidia Serikali ya Rais Samia suluhu Hassan alieanzisha mikopo hiyo kwa nia njema ya kuwainua wanawake.
“Sasa hivi hii mikopo ya wakinamama imesimamishwa, ili kufanya maboresho na kushughulikia changamoto zilizokuwepo hapo awali, na tumeona Rais wetu amesimama kidete na kusema wanawake wapatiwe nyenzo na zana mbalimbali za uzalishaji mali katika vikundi vyao, na sasa Mama yetu Samia hatulii tena kwa ajili yetu wakina mama wa Tanzania,” amesema Mhe.Kabati.
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi