Na Joyce Kasiki, Dodoma
MBUNGE wa Rombo kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joseph Selasini, ametangaza kukihama chama hicho na kujiunga na NCCR-Mageuzi.
Uamuzi huo wa Selasini umekuja ikiwa ni siku moja tangu alalamikie kuondolewa kwenye kundi la WhatsApp la wabunge wa chama hicho bila kuelezwa sababu.
Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dodoma, Selasini amesema atahama rasmi CHADEMA mara baada ya Bunge la Jamhuri ya Muungano kuvunjwa Juni 30, mwaka huu.
Mbunge huyo ametumia fursa hiyo kukiomba chama chake kipya cha NCCR Mageuzi kimpe nafasi ya kugombea ubunge katika Jimbo la Rombo katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Okotoba, mwaka huu ambalo analiongoza hivi kupitia CHADEMA.
Kwa habari za kina soma Gazeti la Majira kesho.
More Stories
DC Korogwe awataka viongozi wa vijiji kuwatumikia wananchi kwa uadilifu
Premier Bet yamtangaza mshindi mkubwa
Dkt. Kazungu atembelea miradi ya umeme Dar es Salaam