November 7, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge Bonnah atoa agizo wanafunzi Segera kwenda shule

Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online

MBUNGE wa Jimbo la segerea Bonnah Ladslaus Kamoli ametoa agizo kwa Serikali kuwafatilia wanafunzi wote wa kidato cha kwanza ambao mpaka sasa hawajafika shuleni kuanza elimu ya sekondari.

.Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli ,alitoa agizo hilo katika ziara yake ya kawaida ya sekta ya Elimu , kuangalia maudhulio ya wanafunzi walioripoti shuleni na miundombinu ya sekta ya Elimu, ambapo alifanya ziara kata ya BONYOKWA, Liwiti na Mnyamani

“ziara yangu hii ya kawaida nimeanzia shule ya sekondari ya Bonyokwa nayo imepokea wanafunzi wa kidato cha kwanza na sekondari ya Liwiti ni shule ya pili nimeona katika taarifa yenu ya shule sekondari ya Liwiti inaeleza idadi ya wanafunzi 400 mpaka sasa hawajafika shuleni naagiza Serikali Halmashauri ya jiji kufatilia kujua wanafunzi hao wapo wapi ili waje kusoma na kama hawapo wameenda wapi wakati wamepangwa katika shule hii” alisema Bonah.

Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Samia Suluhu Hassan inatekeleza Ilani kwa vitendo katika sekta ya elimu imejenga shule za msingi na sekondari katika jimbo la segerea ili watoto waweze kupata elimu bora

Aliwataka Wazazi kuwapeleka watoto shule ili wakapate elimu bora waje kusaidia Taifa .

Aidha katika ziara ya Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli pia alitembelea Shule ya Sekondari ya Bonyokwa kuangalia miundombinu ya shule hiyo ambapo alikuta changamoto ya uzio wa shule na changamoto Photocopy Mashine kwa ajili ya kudurufu mitihani ya majaribio ambapo aliomba uongozi wa shule hiyo kuandika barua kwa ajili ya Photocopy mashine.

Mkuu wa shule ya sekondari Liwiti Wilaya ya Ilala Daudi Ng’wandu alisema wanafunzi wa kidato cha kwanza waliopangwa katika shule hiyo 820 ambao wamefika shule mpaka sasa wamechukua fomu 500 na ambao wameanza masomo wapo Darasani idadi yao 420 wanafunzi 400 bado hawajaripoti katika shule hiyo.

Mkuu Daudi Ng’wandu alisema shule ya sekondari Liwiti jengo la kwanza lilianza Juni 2022 madarasa 20 na matundu ya vyoo 45 wanafunzi wanaosoma shule za jirani watarejea Liwiti 370 wa kidato cha kwanza .

Katika hatua nyingine Mbunge Bonnah Ladslaus Kamoli alisema kero ya Barabara za ndani katika jimbo la segerea zinatarajia kupatiwa ufumbuzi wake hivi karibuni zinatarajia kujengwa Barabara za kisasa katika mradi wa kuboresha miundombinu ya jiji la Dar es Salaam tenda imeshatangazwa katika mfumo mara baada kupatikana wakandarasi Barabara zitajengwa hivyo wananchi wawe na subira kilio cha barabara mbovu kinapatiwa ufumbuzi.