Na Heri Shaaban, TimesMajira Online
MBUNGE wa Jimbo la Segerea Bonah Kamoli, amesema SERIKALI inatarajia kujenga Barabara za kisasa katika mradi wa kuboresha Miundombinu ya jiji la Dar Salaam (DMDP) katika mwaka wa FEDHA 2022 /2023
Mbunge Bonah aliyasema hayo katika ziara yake Jimboni Segerea kutatua kero za wananchi Segerea na Kinyerezi leo.
“Katika kikao cha Bajeti kinachoendelea Dodoma nilielezea suala la Barabara zilivyo kero Jimbo la Segerea ,Bajeti ya Mwaka wa fedha 2022 /2023 ambayo inaanza mwezi June mwaka huu barabara za Kata ya Segerea zilizopo katika Mradi wa DMDP zitaanza kujengwa kwa kiwango Cha lami Pamoja na Taa za Barabarani “alisema Bonah
Mbunge Bonah Ladslaus Kamoli alitaja moja ya Barabara korofi ambayo ipo katika Mradi wa DMDP ni Chang’ombe – Kundy -Mbuyuni nayo ipo kwenye mpango huo kama ilivyo ainishwa kwenye mapendekezo na Diwani wa Kata hiyo na Diwani Robert Manangwa.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya SEGEREA Robert Manangwa alisema Barabara ya Changombe kwa -Kundy -Machimbo hadi Mbuyuni ipo kwenye mipango ya kutengenezwa kwa kiwango cha lami lakini wakati tunaendelea kusubiri budget hiyo ,Tayari wameianisha kwenye budget ya Tarura ili iendelee kukarabatiwa kuondoa usumbufu kwa wananchi.
DIWANI ROBERT MANANGWA aliongeza kwa kusema “Mkandarasi ambaye atapangiwa Barabara hiyo ni vyema akaangalia maeneo korofi ili wayatengeneze vizuri kuondoa usumbufu kwa wananchi”
Mhandisi wa TARURA Wilaya ya Ilala Joseph Sililo alisema tenda ya Barabara kwa ajili ya matengezo ya Barabara hiyo na nyingine ambazo ziko kwenye mpango wa TARURA Wilaya ya Ilala wameshatangaza kuanzia leo kwenye mfumo na kuanzia mwanzoni mwa mwezi wa Saba ukarabati utaanza mara moja!!
More Stories
CCM imejipanga kushinda kwa kishindo
Wanaotumia lugha za matusi,kashfa kwenye kampeni waonywa
Polisi Mbeya yawataka waandishi wa habari kutoa taarifa sahihi