Na Doreen Aloyce,TimesMajira Online,Dodoma
Mbunge wa Jimbo la Mwanakwerekwe Visiwani Zanzibar Khasimu Hassan Haji ameishukuru serikali kupitia Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt.Hussein Ali Mwinyi kwa jinsi walivyoleta miradi ya maendeleo pamoja na miundombinu jimboni kwake jambo ambalo limesaidia kuinua uchumi wa Zanzibar.
Kauli hiyo ameitoa Bungeni Dodoma wakati alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari juu ya maendeleo yaliyopo jimboni kwake kutokana na uchapakazi wa serikali tofauti na hapo awali .
Amesema kuwa kupitia fedha ya Uviko-19 iliyoletwa na Rais Samia i imeweza kujenga shule ya msingi ya ghorofa moja , mradi mkubwa wa maji na soko kubwa la kisasa.
Pia amesema uwepo wa miradi hiyo inaenda kusaidia wananchi kuondokana na adha kubwa ya maji iliyokuwa ikiwakabili sambamba na watoto wao kupata elimu bora tofauti na hapo awali ambapo hapakuwa na shule za kutosha.
Ambapo kwa sasa watoto wanasoma katika mazingira mazuri, wananchi wanapata maji na hata barabara zinaendelea kukarabatiwa jambo ambalo litasaidia kuwa na usafiri wa uhakika wakati wa masika.
Kwani wakati anaingia madarakani alikuta Jimbo hilo linakabiliwa na changamoto za mbalimbali ikiwemo shule ya sekondari na msingi , ubovu wa barabara za ndani,ukosefu wa maji salama na ufinyu wa soko ambalo linajengwa la kisasa kwa sasa.
“Nina kila sababu ya kuishukuru Serilali yetu Rais Samia Suluhu Hassan na Dkt.Hussein Mwinyi kwa kutuletea maendeleo makubwa wananchi wa Jimbo la Mwanakwerekwe, uwepo wa soko la kisasa jimboni kwangu la mwanakwerekwe litasaidia kuinua uchumi wa Zanzibar na biashara kwa ujumla na changamoto zilizopo mi ndogondogo za watu binafsi. “amesema.
More Stories
TASHICO,yatoa ufafanuzi Mv.Serengeti kutitia upande mmoja
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua