Na Penina Malundo,timesmajira,online
MBUNGE wa Jimbo la Kigamboni,Dkt.Faustine Ndugulile amesema uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassani wa kuamua mabinti waliopata ujauzito wakiwa shuleni ni uamuzi mzuri na sahihi katika kusaidia Maisha ya Watoto hao wakike.
Pia amesema takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 27 ya mabinti kati ya umri wa miaka 15 hadi 19 ni wajawazito au tayari wanawatoto.
Akizungumza hayo juzi jijini Dar es Salaam,katika Mahafali ya kwanza ya Taasisi ya kuwawezesha wasichana katika kuwainua kimaendeleo (WEEDO),Dkt.Ndugulile amesema uamuzi huo utasaidia vijana wengi wa kike ambao bado ni wadogo katika kusoma tena na kuja kutimiza ndoto zao walizokuwa nazo mwanzo.
Amesema suala la ujauzito kwa Watoto wa kike ni janga kwa baadhi ya mikoa mingine ambapo kati ya Watoto kuanzia 12 hadi 15 wapo katika hali hiyo.
“Nilipokuwa Naibu Waziri wa Afya niliwahi kutembelea Mkoa wa Katavi, unakuta waliopo wodi ya kujifungulia,asilimia kubwa unakuta ni watoto kuanzia miaka 12 hadi 15,” amesema na kuongeza
“Uamuzi huu wa Rais Samia utasaidia watoto hawa kujikwamua kiuchumi na kujikwamua kielimu,” alisema Aidha Dkt. Ndugulile aliwataka wahitimu hao kuhakikisha wanatimiza ndoto zao na kuzifanya ziwe za kweli katika kuwasaidia kujikomboa kiuchumi.
Amesema wazazi au walezi wa Watoto hao wanatakiwa kuwasaidia kuwasapoti Watoto hao wanapokuwa nyumbani kujiendeleza ili wasiweze kuingia katika vishawishi.
“Taasisi hii imekuwa msaada mkubwa kwa vijana hawa wa kike wanaoishi katika mazingira magumu huku kigamboni kwa kujaribu kuwapa elimu na kuwawezesha ili kuweza kumudu na kuendesha Maisha yao,”amesema
“Huu ni utaratribu mzuri kwa vijana hawa kwani wanajifunza masomo ya Kiingereza,Kushona na mambo mengine na hivi vyote ni kusaidia vijana hao katika kujikwamua kiuchumi,” amesema
Kwa Upande wake Mkurugenzi WEEDO,Rehema Konzo amesema mahafali hayo ni ya kwanza kufanyika katika taasisi yao ambapo takribani vijana wakike 26.
Amesema watoto hao wanatoka katika familia ya kimasikini ni wale ambao Maisha ni magumu hawakupata nafasi ya kwenda shule na wasichana wadogo.
“Kwa Tanzania wasichana kama hawa umri wa miaka 15 hadi 24 ndio ambao maambukizi ya ukimwi yapo kwa kiwango kikubwa,tunafurahi kwa wao kupata fursa ya kusoma kwa mwaka mmoja na kujifunja masomo yote ya ujasiliamari,kiingereza,hesabu na kompyuta,”amesema
Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Tabasamu kutoka nchini Denmark,Eika Dieterich amesema Shirika lao limekuwa likilisaidia shirika la WEEDO tangu mwaka 2017 walipokutana na Mkurugenzi wa WEEDO.
Amesema sasa wanamiaka minne tangu kuwasaidia na kufanya kazi nao katika kuwasaidia vijana hao.
More Stories
Kiswaga:Magu imepokea bilioni 143, utekelezaji miradi
Zaidi ya milioni 600 kupeleka umeme Kisiwa cha Ijinga
Kamishna Hifadhi ya Ngorongoro atakiwa kupanua wigo wa Utalii nchini