Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
SERIKALI imesema itaendelea kukarabati shule chakavu za msingi na sekondari zikiwemo za wilaya ya Misenyi kadiri ya upatikanaji wa fedha .
Aidha, katika mwaka wa Fedha 2025/26, Serikali imetenga shilingi 60,000,000 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba chakavu vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Lugoye.
Naibu Waziri,Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Zainabu Katimba kufuatia swali la Mbunge wa Kuteuliwa Liberata Mulamula ambaye alitaka kujua Mpango wa Serikali wa kukarabati shule kongwe za msingi na sekondari wilaya ya Misenyi
Katika swali la nyongeza Mulamula aliiomba Serikali kufanya tathimini ya hali ya majengo hayo hususan shule ya msingi ya Novati Mtageluka iliyopo Kijiji Cha Kitobo ambayo hali yake ni mbaya sana na inahatarisha maisha ya wanafunzi.
“Naomba shule hii ipewe kipaumbele maana hali yake ni mbaya na miundombinu imechakaa sana ,Serikali itupie jicho ikibidi Naibu Waziri aende akaone hali halisi”amesema Mulamula
Katika hatua nyingine Katimba amesema ,Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi ina shule kongwe 55 zikiwemo shule za msingi 52 na sekondari tatu.
“Kutokana na hali ya miundombinu ya shule hizo kuwa chakavu, Serikali imeendelea kuboresha miundombinu kwa kukarabati au kujenga miundombinu mipya kwa awamu ambapo , mwaka 2023/24 na 2024/25 Serikali imetumia shilingi 182 kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa kwenye shule 11 na ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule tano katika Halmashauri ya Wilaya ya Misenyi
More Stories
Rais Samia amteua Mkurugenzi Mtendaji TANESCO
RMO,DMO waagizwa kumsimamia Mkurugenzi ununuzi vifaa ,vifaa tiba
Mgogoro wa mipaka Ushetu,Kaliua watua Bungeni