Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma
KATIKA mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetenga shilingi milioni 625 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la wazazi, jengo la upasuaji, jengo la maabara, jengo la kuhifadhi maiti na kichomea taka Kituo cha Afya kazuramimba katika Halmashuri ya Wilaya ya Uvinza.
Hayo yamesemwa Aprili 15 mwaka huu Bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt.Festo Dugange wakati akijibu swali la Mbunge wa Kigoma Kusini Nashon Bidyanguze ambaye katika swali la msingi alitaka kujua lini Serikali itapeleka fedha kujenga majengo katika Kituo cha Afya Kazuramimba – Uvinza.
Aidha katika swali la nyongeza Mbunge huyo alitaka kujua lini Serikali itapeleka fedha ilizoahidi kiasi cha shilingi milioni 150 kwenye kituo Cha Afya Nguruka ambacho kimechakaa na Waziri Mkuu alishafika kituoni hapo kuhakikisha uchakavu huo wa kituo.
Pia alitaka kujua lini fedha zitapelekwa katika Vituo vya Afya vya Kalya,Buhingu,Ilagala na Uvinza ambavyo miundombinu yake haijakamilika kama wodi na majengo mengine.
Akijibu maswali hayo Dkt.Dugange amesema Kituo cha afya Kazuramimba katika Halmashauri ya Uvinza kinahudumia wananchi wapatao 40,711.
Aidha amekiri kwamba Moja ya vituo vya Afya kikiwemo Cha Nguruka ni Moja Vituo vinavyohitaji kuongezewa majengo na kwamba lilikuwa ni agizo la Waziri Mkuu huku akisema maagizo ya viongozi wa Kitaifa ni kipaumbele namba Moja katika utekelezaji.
“Namuhakikishia Mheshimiwa Mbunge kwamba tayari tumeshaweka katika Mpango wa fedha za Mfuko wa Dunia na tunatarajia kupeleka fedha hizo Nguruka mapema iwezekanavyo mwishoni mwa mwaka huu 2024/2025 au mwanzoni mwa mwaka 2025/2026.”amesema Dkt.Dugange
Kuhusu uhaba wa miundombinu katika Vituo vya Afya amesema,Serikali inafahamu Kuna Vituo vyenye upungufu wa miundombinu na kwamba Serikali imeweka kwenye mpango na tayari awamu ya kwanza imeshaanza .
“Kwenye awamu ya pili tutahakikisha Vituo hivyo vinne tunavipa kipaumbele katika kumalizia majengo yanayohitajika.”amesisitiza Dugange
More Stories
Wazee wawili jela maisha kwa kubaka na kulawiti
Dkt.Biteko aongoza waombolezaji mazishi ya Mkurugenzi Mtendaji TANESCO
Nyongo: Sekta binafsi ina mchango mkubwa kwa taifa