December 25, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbunge achangia ujenzi ukumbi wa CCM

Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Simanjiro

Mkurugenzi wa Kampuni ya Franone Mining Gems Ltd Onesmo Mbise ametoa sh.Mil.30 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ukumbi wa Mikutano wa CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, ambapo wanachama wa CCM wamempongeza kwa uchangiaji huo.

Harambee hivyo iliendeshwa juzi na Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo katika Ofisi ya CCM Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, alipokua ziara ya kikazi Wilayani humo, baadhi ya wananchama wamesema ukumbi huo una zaidi ya miaka 10 haujaendelezwa, hivyo ujio wa Katibu huyo Mkuu ni wa mafanikio makubwa Wilayani Simanjiro.

Akizungumza na gazeti la Majira Mbise alisema ametoa mchango wa sh.mil.30 ili kuunga mkono jitihada za Serikali ya Chama Cha Mapinduzi ( CCM ) chini ya Mwenyekiti wake Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

” Chama chetu pendwa Cha CCM ndio kimeweka Serikali Madarakani, hivyo na Kampuni ya Franone Mining Gems Ltd nayo ni miongoni mwa tunaotekeleza ilani ya Ccm Kwa vitendo” amesema Mbise.

Aidha alisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan imefanya mambo mengi na makubwa kwa Taifa hili la Tanzania, ikiwemo kuweka miundombinu mizuri ya shule, Barabara, vituo vya afya na Mengine mengi.

Kufuatia hayo kama Kampuni ya Franone imeona ni vema nayo ikaunga mkono jitihada hizo Kwa kuchangia sh.mil. 30 Kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa CCM Wilaya ya Simanjiro.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Wilaya hiyo Amos Shimba aliwataja wenginen waliochangia kuwa ni Bilionea Laizer sh.mil.20, Sanare Sailep ( Mula) sh.mil.15, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Simanjiro Kiria Ormemei Laizer sh.mil.5, Mbunge wa Jimbo hilo Christopher Ole Sendeka sh.mil.6.

Aidha wengine waliunga mkono jitihada hizo ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Manyara Peter Toima amechangia bati 100, Mjumbe wa Mkutano Mkuu CCM Taifa Daniel Matery sh.mil.2, Diwani wa Kata ya Loiborsiret Ezekiel Lesenga amechangia sh.mil.1, Mwenyekiti wa Loiborsoit Lengai amechangia sh.mil.1, Edward Loure sh.mil.1.

Aidha Shimba alifafanua kuwa wengine waliochangia saruji ni pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Manyara mifuko 100 ya saruji, Katibu Mwenezi Taifa Sophia Mjema mifuko 50, Issa Gavu Katibu wa Organization mifuko 50.

“Wengine waliochangia ni Mkuu wa Wilaya ya Kiteto Mbaraka Al Haji Batenga mifuko 25, Wabunge wa viti Maalum Mkoani Manyara Regina Ndege mifuko 40 na huku Yustina Rahhi akichangia mifuko 50, Mh.Regina Ndege mifuko 40 ” alisema Shimba.

Katibu Shimba alimshukuru Katibu Mkuu CCM Daniel Chongolo kwa kuendesha harambee hiyo Kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa ukumbi huo, ambapo jumla ya fedha zote ni sh.mil.81.

Hata hivyo Shimba alisema mlango wa kuendelea kuchangia ujenzi huo uko wazi, ili wale wengine wanaokipenda Chama kama madiwani, viongozi wengine mbalimbali waweze kuendelea kuchangia.

Wakiongea Kwa nyakati tofauti wakereketwa na wanachama wa CCM walisema ukumbi huo una miaka zaidi ya 10 bado haujakamilika, hivyo wanampongeza Mkurugenzi wa Kampuni ya Franone Mining Gems Ltd Onesmo Mbise na Bilionea Laizer pamoja na wengine waliojitoa kuchangia ujenzi wa ukumbi huo.