Na Mwandishi Wetu, TimesMajira Online
MSANII wa muziki wa Bongo fleva kutoka lebo ya WCB Mbwana Kilungi, maarufu kama ‘Mbosso’, amelia na matapeli wa mitandaoni baada ya matapeli hao kutapeli watu kwa kutumia akaunti yake ya Facebook ambayo ni feki.
Akiweka wazi hilo kupitia kwenye akaunti yake ya Instagram Mbosso amesema, kuna jamaa anawaibia watu kwa kujifanya yeye ndio Mbosso kwa kutumia akaunti fake, hivyo ni vyema watu wengi wakachkua tahadhari.
“Tafadhali fikisha taarifa hizi kwa mashabiki zangu pendwa wanaomtumia Mtandao wa Facebook. Kila Siku napokea taarifa za watu wanaoiba kutumia jina langu. Kuna jamaa anawaibia sana watu kujifanya yeye ndio Mbosso, ni huyo mwenye Account ya Mbosso iliyoandikwa Fake upande wa kushoto. Hiyo sio akaunti yangu ya Facebook na wala haipo chini yangu
“Page yangu ya Facebook ni hiyo iliyoandikwa Original upande wa kulia Mbossokhan.
Epuka matapeli wa mitandaoni,” alisema Mbosso.
More Stories
Startimes yazindua makala ya China, Africa
Mwanasheria wa Katavi aliyetimkia kwenye muziki achaguliwa tuzo za MIEMMA
Coca-cola ‘Kitaa Food Fest’ yahitimishwa kwa mafanikio