April 16, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbogo aomba Tume kuchunguza madai ya waliokuwa wafanyakazi wa EAC

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Dodoma

SERIKALI imesema,waliokuwa wafanyakazi wa lilikokuwa Shirika la Posta na Simu Tanzania pamoja na Shirika la Reli la iliyokuwa Jumuiya ya Afrika ya Afrika Mashariki (EAC) walilipwa mafao ya mkupuo kupitia Ofisi ya Mlipaji Mkuu wa Serikali mwaka 2005.

Hayo yamesemwa Bungeni Leo Aprili 15 ,2025 na Waziri wa Fedha Dkt.Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la msingi la Mbunge wa Viti Maalum Taska Mbogo aliyetaka kujua ni lini Serikali itawalipa waliokuwa Wafanyakazi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hata hivyo Dkt.Nchemba amesema, baada ya malipo hayo baadhi yao walirudi kudai mapunjo ambapo Wizara iliyafanyia kazi kulingana na taratibu na kwamba Mwaka 2009 Serikali iliwarejesha Wastaafu hao kwenye Daftari la Pensheni ambapo wanalipwa kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina.

Kwa mujibu wa Waziri huyo, Wastaafu hao kwa sasa wanalipwa Pensheni yao ya kila mwezi kwa utaratibu wa miezi mitatu mitatu huku akisema,hadi sasa Serikali imelipa pensheni ya kipindi cha Aprili, 2025 hadi Juni, 2025 kiasi cha Shilingi bilioni 1.085 kwa wafanyakazi 1,794 wa yaliyokuwa mashirika ya EAC ya TTCL (629), TRC (792), TPC (252) na TPA (8).

Katika swali la nyongeza Mbogo ametaka kujua kama Serikali ipo tayari kukaa na Taasisi nyingine zilizokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki ukiacha mbili alizozitaja Waziri Nchemba Ili kuangalia madai yao .

“Kwa kuwa waliokuwa wafanyakazi wa EAC iliyovunjika mwaka 1977 ,wanadai Serikali iliwalipa pesa pungufu na haikufuata tathimini iliyotolewa ,je Serikali ipo tayari kuunda Tume na kukaa na wafanyakazi hawa Ili kupata muafakabwa kulipa fedha zao?”amehoji Mbogo

Akijibu maswali hayo Dkt.Nchemba amesema Serikali imepokea wazo la kukaa na Taasisi nyingine zilizokuwa EAC .

Aidha kuhusu mapunjo yao amesema ,Serikali imelichukua huku akisema utaratibu wa Serikali kulipa madai na madeni pindi yanapojitokeza Huwa yanafanyiwa uhakiki na hoja Huwa zinaangaliwa na Mdhibi na Mkaguzo Mkuu wa Serikali ,Mwanasheria Mkuu wa Serikali ,Mkaguzi wa Ndani na Idara nyingine zinazoshighulikia masuala ya aina hiyo.

“Hivyo tunalipokea na Serikali itafanyia kazi maeneo yote mawili.”amesisitiza Dkt.Nchemba