December 22, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mbeya kutumia vituo 1,577, uboreshaji daftari la kudumu

Na Esther Macha Timesmajira Online, Mbeya

MKURUGENZI wa Uchaguzi ,Kailima Ramadhani amesema,Mkoa wa Mbeya una jumla ya vituo vya kuandikisha wapiga kura 1,577, ambavyo vitatumika kwenye uboreshaji wa daftari la kudumu la mpiga kura,kwa mwaka 2024,,ikiwa ni ongezeko la vituo 66, katika vituo 1,511 vilivyotumika kwenye uboreshaji mwaka 2019/20.

Huku Mkooa wa Iringa kuna vituo 1,367 ambavyo vitatumika kwenye uboreshaji wa daftari kwa mwaka 2024, ikiwa ni ongozeko la vituo 140, katika vituo 1,227 vilivyotumika kwenye uboreshaji wa daftari mwaka 2019/20.

Ramadhani amesema hayo Desemba 15 ,2024 wakati akiwasilisha mada kwa wadau wa uchaguzi mkoani Mbeya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi Jaji wa Mahakama ya Rufaa Jacobs Mwambegele,amesema kuwa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika Mikoa ya Iringa, Mbeya na Dodoma katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa umepangwa kuanza,Desemba 27 mwaka huu na kukamilika Januari 2,2025 huku vituo vikifunguliwa kuanzia saa 2:00 hadi saa 12:00.

Ameongeza kuwa pindi zoezi hilo katika Mikoa ya Iringa na Mbeya litakapokamilika,Tume itakuwa imekamilisha mzunguko wa nane kati ya mizunguko 13 ya uboreshaji wa daftari hilo,ambapo tangu kuzinduliwa kwa zoezi hilo Julai 20,2024,Tume imefikia na kukamilisha zoezi hilo kwa mikoa 21.

Ameitaja mikoa hiyo kuwa ni Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma na Singida,Mikoa ya Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba na Kaskazini Pemba iliyopo Zanzibar.

Ameongeza kuwa hivi sasa uboreshaji wa daftari hilo,unafanyika katika mikoa miwili ya Arusha na Kilimanjaro na Tume inatarajia kukamilisha zoezi hilo katika mikoa hiyo mnamo Desemba 17,2024.