January 8, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mawaziri SMT na SMZ wakutana Zanzibar kujadili masuala ya muungano

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Saada Mkuya akiongoza kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss – Abdul Wakil leo tarehe 23/08/2021. Wa pili kutoka kushoto ni Mwenyekiti Mwenza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo na Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga. Kulia ni Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Thabit Faina
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Selemani Jafo akizungumza katika kikao cha Mawaziri wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano (SMT) na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) kilichofanyika katika Ukumbi wa Sheikh Idriss – Abdul Wakil leo 23/08/2021. Wengine katika picha ni Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Mhe. Saada Mkuya, Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi. Mary Maganga na kulia ni Katibu Mkuu Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais Bw. Thabit Faina
Mawaziri wa SMT Prof. Adolf Mkenda, Prof. Palamagamba Kabudi na Dkt. Mwigulu Nchemba wakifuatilia mjadala katika kikao cha SMT na SMZ katika Ukumbi wa Idriss Abdul-Wakil, Zanzibar.