January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mawakili wa Serikali watakiwa kujielimisha

Na Zena Mohamed,Timesmajira Dodoma

MWANASHERIA Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi amewataka Mawakili wa Serikali nchini kuendelea kujielimisha kila siku kutokana na kukua kwa taaluma ya Sheria Ulimwenguni kulingana na umuhimu wa kazi yao wanayoifanya ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi.

Profesa Kilangi ametoa wito huo jijini hapa leo wakati akifungua mafunzo ya siku nne kwa Mawakili wa Serikali yenye lengo la kuwaongezea uwezo katika stadi za uendeshaji madai ya usuluhishi kwa kuwapa ujuzi ambayo yameandaliwa na Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.

Amebainisha kuwa, mafunzo hayo ni muhimu na yatasaidia kuwanoa Mawakili hao ili kuendana na mabadiliko ya taaluma ya sheria ambayo yamekuwa yanatokea kila siku ulimwenguni.

“Niishukuru sana ofisi ya Wakili mkuu wa Serikali kwakuandaa mafunzo haya ambayo ni muhimu na yatawapa uwezo na kuongeza ufanisi wa utendaji kazi kwa mawakili kwa lengo la amslahi ya umma.

“Haya yote ni maeneo muhimu sana sababu ya mabadiliko katika majukumu yenu na wengi wenu mtashirikiana na wakili mkuu wa serikali kwaajili ya kusimamaia kesi hasa za serikali ndani na nje ya nchi hivyo ni lazima muwe na ujuzi ya kuweza kusimamaia mashauri hayo.

“2019 tulilazimika kuendesha kesi mbele ya mahakama kuu ya biashara London uingereza ndani ya mwezi mzima,ni lazima tuweze kuendesha hizi kesi ndani na nje ya nchi kutokana na wigo kuongezeka,”amesema Kilangi

Amesema, mafunzo hayo yataongeza uwezo na weledi katika suala zima la usuluhishi na madai mbalimbali hivyo waendelee kujielimisha kuhusiana na changamoto mbalimbali.