November 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Mavunde aipongeza NIC kwa utoaji huduma za bima,ataka elimu hiyo iwafikie wakulima wengi zaidi

Na Joyce Kasiki,Timesmajira online,Mbeya

NAIBU Waziri wa Kilimo Anthony Mavunde ameliasa Shirika la Bima la Taifa ( NIC) kuhakikisha wanawafikia  na kutoa elimu ya bima kwa wakulima ili wawze kujiunga na Bima ili waitumie ipasavyo pindi wanapokumbwa na majanga mbalimbali.

Akizungumza alipotembelea banda la NIC katika maonyesho ya wakulima Nane Nane jijini Mbeya,Mavunde amesema,huu ni wakati muafaka sasa kwa wakulima kujiunga na huduma huduma hiyo.

“Nimetembelea katika banda la NIC katika maonyesho haya na nimejionea  kazi na huduma wanazotoa,Shirika hili ni moja ya mashirika makubwa yanayotoa huduma hizi kwa muda mrefu sana,kwa hiyo sasa ni muda muafaka kwa watanzania kupata elimu ya masuala ya bima ili kuhakikisha kwamba wanaitumia bima ipasavyo katika majanga mbalimbali.”amesema Mavunde na kuongeza kuwa

“Na sisi pia kwenye kilimo tumeweka msisitizo kuhakikisha wadau wwetu ambao ni wakulima  wanajiunga na mfumo wa bima kama sehemu ya kuwakinga na majanga mbalimbali.”

Amesisitiza kuwa wanakulima wanapaswa kufikiwa katika maeneo yao na kupatiwa elimu hiyo lakini pia Shirika hilo liwafikie wakulima moja kwa moja ili kujua huduma wanayoihitaji ili waweze kunufaika na huduma za shirika hilo pindi wanapopata majanga mbalimbali yanayohusu masuala ya kilimo.

Awali akizungumza na waandishi wa habari katika banda hilo Afisa Uhusiano wa NIC Ephrasia Mawalla amesema,NIC wamebobea katika kutoa huduma za Bima na kuwafidia pale wanapopata majanga mbalimbali katika nyanja tofauti kama vile bima ya mazao,mifugo ,nyumba,safari,magari,maisha na mazao.

Afisa Uhusiano wa NIC Ephrasia Mawalla akionyesha huduma zinazotolewa na Shirika hilo.

“Katika bima ya mazao na mifugo humsaidia mkulima kumkinga na majanga ambapo katika mifugo tunaangalia vifo,magonjwa ya mifugo na hasara inapotokea katika eneo hilo inabebwa na Bima.”amesema Mawalla na kuongeza kuwa

“Pia tunaangalia changamoto za wadudu ,ukame,mafuriko,kimbunga na mvua yam awe hivyo vyote vinapomkumba mwanachama wetu anafidiwa na Shirika hasara inayopatikana na Shirika letu humfidia mwananchama ndani ya siku saba tangu kutokea kwa tukio husika.”  

Aidha Mawalla amesema  wapo katika maonyesho ya wakulima Nane Nane kutoa elimu ya Bima wananchi wengi zaidi waweze kujiunga kwa maslahi yao.

Naye Mratibu wa Bima za Mazao na Mifugo kwa zaidi ya miaka 59 na katika kipindi chote hicho Shirika limekuwa likitoa huduma za Bima pamoja na kushauri wananchi katika eneo hilo.