January 22, 2025

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Wafanyakazi wahamiaji wakiwa wamejipumzisha kwenye mabomba ya saruji kwa ajili ya kujengea makaravati, baada ya kusikia taarifa za kuongezeka muda wa kukaa ndani ikiwa ni tahadhari dhidi ya virusi vya corona (COVID-19) mjini Lucknow, India juzi. (Picha na REUTERS)

Matukio ya wiki duniani (picha)

Waumini wakifanya sala katika Msikiti wa Sindh uliopo jimboni Karachi, Pakistan Aprili 19, mwaka huu huku wakiwa wamezingatia kanuni ya kuacha nafasi kati ya mtu na mtu, Taifa hilo linaendelea na amri ya kutotoka ndani ikiwa ni tahadhari ya kujikinga na maambukizi ya virusi vya corona (COVID-19).(Picha na EPA-EFE).
Vijana raia wa Misri wakishirikiana kuipamba mitaa yao ikiwa ni maandalizi ya kuanza Mwezi Mtukufu wa Ramadhani wilayani Hadayek el-Maadi mjini Cairo juzi. (Picha na AFP).
Maafisa wa Polisi nchini India wakiwa wamevalia vazi maalum la kujikinga dhidi ya virusi vya corona mjini Mumbai juzi, huku wakiendelea kuimarisha ulinzi wakati taifa hilo likiendelea na zuio la kukaa ndani kwa raia wote. (Picha na EPA-EFE).
Mfanyakazi wa mgahawa wa McDonald Kallang akimjulisha mteja wao juu ya kusitishwa kwa huduma kwa muda. Matawi yote ya kutoa huduma ya chakula cha haraka ya McDonald nchini Singapore yamefungwa hadi Mei 4, mwaka huu baada ya wafanyakazi saba kupimwa na kugundulika wana virusi vya corona (Covid-19) hivi karibuni. (Picha na DESMOND WEE/ST).