Na Mary Margwe, TimesMajira Online, Ruangwa
Kampuni ya Madini ya Elianje Genesis Kampani Limited tayari imeanza kupata mafanikio makubwa kupitia Kongamano la Madini na Fursa za Uwekezaji lililofayika hiki karibuni Wilayani Ruangwa, na hivyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Talack Kwa kuwa na maono ya kuanzisha Kongamano lililokua nantija kwao.
Pongezi hizo zimetolewa Jana na Meneja wa Kampuni ya Madini ya Elianje Genesis Kampani Limited Philbert Simon Massawe wakati alipokua akizungumza mbele ya waandishi wa vyombo mbalimbali vya Habari waliotembelea kujionea namna ambavyo Mgodi huo unaendesha shughuli zake katika maeneo ya Namungo Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi.
Massawe amesema kufanyika kwa kongamano la Madini na Fursa za Uwekezaji lililofayika hivi Karibuni katika Viwanja vya Soko Jipya Kilimahewa Wilayani Ruangwa Mkoani Lindi kwao kama kampumi ya Elianje Genesis Kampani Limited ni mafanikio makubwa kwani wameonekana, wamejitangaza na wamejulikana na hivyo kupelekea kupata oda nyingi ya Madini wanayozalisha katika Mgodi huo.
“Tunashukuru Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Waziri wa Madini Dotto Mashaka Biteko, Mkuu wa Mkoa huo Zainab Talack kwa kutuletea tamasha hili ambalo kwetu limekua na mafanikio makubwa sana, kwani tumejitangaza, tumejulikana na sasa tunaendelea kupata oda za madini mbalimbali tunayozalisha katika Kampuni yetu ya Elianje Genesis ” amesema Meneja Massawe.
Amesema Mkuu wa Mkoa wa Lindi Zainab Talack ameufanya Mkoa wa Lindi ujulikane nini kipo, na kinatikana wapi , ambapo mwezi mzima karibia ni Mkoa wa Lindi unazungumzia madini tu midomoni mwa wadau mbali mbali wa Madini lakini pia hata kwa wananchi kwa ujumla.
” Siku ya tatu tu ya Maonyesho ya kongamano la Madini na Fursa za Uwekezaji, sisi tayari tumepata wanunuzi wengi wa Madini aina ya Graphite, tayari wengine magari yameondoka baada ya kukamilisha oda zao, hizi zote ni juhudi za Serikali yetu ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, hususani Mkuu wetu wa Mkoani Lindi Zainab Talack aliyekuja na wazo la kuleta tamasha hili kubwa na muhimu kwetu na kwa Taifa kiujumla.
Amesema kutokana na kongamano hilo pia tumepokea email za kutosha zinazohusika kupokea kwa oda mbalimbali ya Madini aina ya copper na mengineyo, hivyo ameipongeza Serikali kwa kuwarahidishia katika upatikanaji wa Soko, kwani bila Serikali kufanya hivyo hadi leo wangebaki walipokua awali.
Akielezea Madini yanayozalishwa katika Kampuni hiyo Massawe amesema yapo Madini aina sita yanayozalishwa ikiwa ni pamoja na Graphite, Nikei, Chuma, Green Garnet, Dhahabu na Copper ambapo amesema kampumi hiyo inapatikana katika eneo la Namungo, pamoja na Namkonjera Wilayani Ruangwa.
More Stories
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu
Airtel yatoa zawadi kwa wateja wake
Mpango ashiriki mazishi ya Mama yake Serukamba