Na Heri Shaaban, TimesMajira Online, Ilala
Madhindano ya Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam yanatarajia kuanza wiki ijayo kila Kata kwa ajili ya kutafuta timu ya Jimbo kila wilaya Ili washiriki mashindano ya Wazazi mkoa Dar Es Salaam Uwanja wa Uhuru Shamba la Bibi .
Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Kamati ya Michezo Jumuiya ya Wazazi mkoa Saady Kimji, ambaye pia Mjumbe wa Mkutano Mkuu Baraza la Wazazi CCM Taifa katika kikao cha Kamati ya Utekelezaji Mkoa alisema mashindano hayo yatashirikisha Kata 102 za mkoa Dar es Salaam.
Mwenyekiti Saady Kimji alisema mashindano hayo yataanzia ngazi ya kila kata kutafuta timu ya Jimbo iweze kushiriki mashindano ya ngazi ya Mkoa .
“Nawaagiza makatibu Kata wote kuandaa timu za mpira miguu katika Kata zenu ndani ya Siku Saba mashindano ya mpira miguu yaweze kuanza na kufuata maagizo ya Jumuiya ya Wazazi Mkoa ” alisema Kimji .
Mwenyekiti Saady Kimji alisema kazi ya maelekezo ya Baraza la Wazazi Mkoa waliopewa wameanza kutekekeza wanaomba wapewe Ushirikiano na kuwa wa moja Ili mashindano yaweze kufanikiwa kila wilaya anzeni kutangaza mashindano haya yameshapata baraka ngazi ya chama.
Alisema dhumuni la Michezo hiyo kuitangaza Jumuiya ya Wazazi na shughuli zake kwa ajili ya kujenga chama kwani katika michezo hiyo watatafuta vipaji vya michezo ,kutoa ajira na kujenga mahusiano na udugu .
Akizungumzia dhumuni lingine la mashindano hayo alisema Jumuiya ya Wazazi inajipanga chama na Serikali katika kuwakikisha CCM Ina shika Dola katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024 na Uchaguzi mkuu wa Rais Wabunge na Madiwani .
Aliagiza Wilaya zote kushiriki kikamilifu kuwakikisha kila wilaya inaleta timu zao katika kinyanganyiro hicho Cha kombe la wazazi mkoa Dar es salaam .
Wakati huo huo Kimji alitoa onyo kwa kata itakayoshindwa kutoa timu katika mashindano hayo itawajibishwa kwa kukwamisha mashindano kwani Kila kiongozi weanatakiwa kupokea maelekezo na kisimamia ukishindwa kisimamia utoshi kurwa kiongozi nafasi yoyote
More Stories
TAG yampongeza Rais Samia
CCM Tabora yamfariji mjane wa kada anayedaiwa kujiua
FDH yaanza kutekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wanawake wenye ulemavu