Na Mwandishi wetu, TimesMajira Online
MASHABIKI wawili wa soka Tanzania wamejishindia jumla ya Sh145, 957, 650 baada ya kubashiri kiusahihi zaidi jumla ya mechi 12 katika mchezo wa kubahatisha wa Perfect 12 wa kampuni ya michezo ya kubah M-Bet Tanzania.
Meneja Masoko wa kampuni ya M-Bet Tanzania, Allen Mushi amesema, washindi hao kuwa ni Juma Makongo ambaye ni mkazi wa Mwananyamala, Dar es Salaam na Juma Mussa Ngua kutoka Mkoa wa Singida.
Washindi hao wametumia Sh1,000 tu kubashiri mechi hizo 12 za ligi mbalimbali hapa duniani na kuweza kugawana kiasi cha fedha hicho.
Amesema, Makongo na Ngua wanakuwa washindi wa nane tokea kuanza kwa mwaka na kampuni yao imetumia zaidi ya Sh milioni 550 kuwazawadia washindi mbalimbali walioweza kubashiri kwa usahihi na kuibuka washindi.
“Tunafuraha kuwazawadia washindi hawa na tunaamini kuwa wataweza kubadili maisha yao kupitia fedha walizoshinda. M-Bet itaendelea kuwa nyumba ya mabingwa,” amesema Mushi.
Akizungumza baada ya ushindi huo, Ngua ambaye ni shabiki wa Simba amesema kuwa hakuamini kupata kiasi kikubwa cha fedha hicho ambacho atasaidia wazazi wake na kuanzisha biashara.
“Mimi ni mmachinga, sikutegemea kupata kiasi kikubwa cha fedha hiki na nitaanza kujenga nyumba kwa wazazi wangu huku nikiboresha biashara,” amesema Ngua.
Mkuu wa Kitengo cha Michezo ya kubahatisha wa Mamlaka ya Mapato wa Mkoa wa kodi wa Ilala, Shaaban Mwanga amewapongeza kampuni ya M-Bet kwa kuwa walipa kodi wazuri hapa nchini na kusema kuwa, michezo ya kubahatisha inachangia kwa kiasi kikubwa sana pato la Taifa.
More Stories
Zanzibar kuzalisha wachezaji wenye vipaji
Othman awakabidhi jezi Zanzibar Heroes
Rais Samia: Yanga endeleeni kuipeperusha bendera ya Tanzania